Na Mwandishi Wetu
DODOMA: NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Maduhu Kazi amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kutambua umuhimu wa Mazoezi katika kuimarisha afya, kuweka watu pamoja hivyo kuimarisha upendo na mshikamano baina ya Watumishi
Dkt. Maduhu amesema hayo alipokua akizindua programu ya Mazoezi kwa Watumishi wa Wizara hiyo iliyofanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Dodoma Mlimani.
Pia ameipongeza Menejimenti ya Wizara kwa kutoa fursa hiyo itakayosaidia kuimarisha na kuboresha afya za watumishi kupitia Mazoezi.
Vilevile amewasisitiza watumishi kutumia nafasi hiyo kushiriki kwenye Mazoezi hayo yatakayokuwa yakifanyika mara mbili kwa wiki kila siku ya Jumanne na Alhamisi kuanzia saa 10 Alasiri
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwasisitiza Watumishi wote kushiriki Mazoezi haya kila wiki kwa watumishi waliopo hapa Dodoma na kwa wale walipo nje ya Dodoma,” amesema.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Hilda Tegwa ameelekeza maeneo yatakayotumika kufanya nazoezi hayo.