MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Biteko Akaribisha Wawekezaji Sekta Ya Nishati
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Biteko Akaribisha Wawekezaji Sekta Ya Nishati
Habari

Biteko Akaribisha Wawekezaji Sekta Ya Nishati

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na  Mwandishi Wetu
NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali inawakaribisha wawekezaji katika sekta ya nishati ili kuongeza kasi  ya uzalishaji, usambazaji na uunganishaji wa wateja katika Sekta ya Nishati nchini.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Oktoba 21, 2024 nchini Singapore wakati akishiriki mjadala kuhusu nishati ambao ulishirikisha Waziri wa Madini na Nishati  wa Cambodia,  Keo Rottanak na Waziri wa Maliasili kutoka New Zeland Shane Jones katika ufunguzi wa Wiki ya Kimataifa ya Nishati nchini Singapore.
“ Serikali haziwezi kufanya kila kitu zenyewe hivyo ni muhimu kushirikiana na sekta binafsi. Sisi Tanzania tunawaalika sekta binafsi ili kuwekeza katika sekta ya nishati kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji, upatikanaji na usambazaji nishati na kuboresha maisha ya watu kwa ujumla,” amesema Dkt. Biteko.
Akizungumzia, ajenda ya nishati safi ya kupikia nchini amesema kuwa ni matokeo ya utafiti uliofanywa na kubaini kuwa idadi kubwa ya Watanzania wanatumia kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia hali inayosababisha magonjwa ya mfumo wa upumuaji na uharibifu wa mazingira.
Ili kupunguza athari hizo, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali imeandaa mkakati unaolenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
“ Serikali imeendelea  kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na kuhakikisha nishati safi inapatikana kwa urahisi na bei nafuu na hivyo tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika hili kwa sababu soko lipo,” amesema Dkt. Biteko.
Aidha, Dkt. Biteko ametaja miradi mbalimbali inayofanywa na Serikali ikiwemo mradi wa kufua umeme wa  Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2115 ambao amesema kukamilika kwake kutaongeza ziada ya umeme nchini.
“ Serikali inaendeleza vyanzo vipya vya nishati mfano umeme wa jua, upepo na gesi, aidha kwa sasa asilimia 51 ya umeme unazalishwa kwa maji. Tanzania tumeendelea na maandalizi ya  kuziuzia umeme nchi za Kenya, Rwanda, Burundi na sasa tunaendelea na mradi kwa ajili ya kuunganisha na nchi ya Zambia, kupitia Umoja wa Mauziano ya Umeme wa pamoja katika nchi za Afrika Mashiriki na Jumuiya za Kusini mwa Afrika (SADC) tuna soko la uhakika na hivyo tunawakaribisha wawekezaji kuja kushirikiana nasi,” amesisitiza Dkt. Biteko.
Naye, Waziri wa Madini na Nishati  kutoka Cambodia,  Keo Rottanak amesema kuwa mwaka 1998 nchi yake ilifanya mageuzi makubwa katika sekta ya nishati na kuwa sasa asilimia 99 ya vijiji vina umeme.
“ Tutahakikisha tunafikisha umeme katika nyumba za watu na malengo yetu ni ifikapo mwaka 2030 tunazalisha umeme kwa nguvu ya jua kama  mbadala wa umeme unaozalishwa kwa nguvu yamaji,” amesema  Rottanak.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na kutoka nchini  New Zeland,  Shane Jones amesema kuwa nchi yake imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kusambaza umeme na kuwa inajikita katika kuwekeza katika vyanzo mbadala vya kuzalisha nishati.
Awali akifungua mkutano huo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Singapore Gan Kim Yong amesema kuwa mahitaji ya nishati duniani yanazidi kuongezeka siku hadi siku hivyo nchi zinapaswa  kubuni vyanzo mbadala na kupunguza madhara yatokanayo na gesi ya ukaa ifikapo mwaka 2050.
Amesema nchi yake imeongeza vyanzo mbadala vya nishati na kuiobgeza kuwa kwa sasa inajielekeza katika matumizi ya Hydrojen .
“ Kwa sasa tuko kwenye mkakati wa kuzalisha umeme kwa kutumia hydrojen na nyuklia ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kuongezeka kwa ushiriki wa Kampuni  za Google na Amazon ambazo zimeonesha nia ya kuwekeza kwenye miradi ya nishati jadidifu.” Amesema  Kim Yong.
Aidha,katika mkutano huo pia umefanyika uzinduzi wa tawi la ofisi ya kanda ya Shirika la  Kimataifa  la Nishati (IEA) nchini Singapore.

You Might Also Like

CCM yavunja rekodi – Makala

Ridhiwani Kikwete Awataka Vijana Kuwa Mabalozi Wazuri wa Amani

Askari wa Jeshi La Uhifadhi Kusini Wakumbushwa Wajibu

Dar es Salaam Kuunda Kamati Ya Kupitia Majengo Chakavu

Tutumie Mitandao Kwa Matumizi Yenye Manufaa – Kilimbe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Jeshi La Uhifadhi Wasisitizwa Kuzingatia Misingi ya Haki za Binadamu
Next Article Kongamano  La Kimataifa La Jotoardhi Laanza Kwa Mafanikio
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?