MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania, Ufini Kushirikiana Teknolojia Za Kisasa Sekta ya Misitu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania, Ufini Kushirikiana Teknolojia Za Kisasa Sekta ya Misitu
Habari

Tanzania, Ufini Kushirikiana Teknolojia Za Kisasa Sekta ya Misitu

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
TANZANIA itapata fursa zaidi ya kuboresha sekta yake ya
misitu inayochangia kwa sasa asilimia 4.2 ya Pato la Taifa (GDP), kufuatia utayari wa Serikali ya Finland (Ufini) na wadau wengine wa teknolojia nchini hapa kusaidiana katika nyanja za teknolojia za kisasa.
Hayo yamesemwa leo  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, mara baada ya kutembelea kampuni na vituo kadhaa vya teknolojia za misitu katika mji wa Joensuun  Ufini unaosifika kuwa kitovu cha sekta ya misitu nchini hapa.
“Tumetembelea kampuni kubwa duniani yaliyoko hapa kama Abounat, John Deere, Business Finland na Kitivo cha Teknolojia za Misitu cha Chuo Kikuu Finland kiitwacho East Finland University,” ameeleza Dkt. Abbasi.
Moja ya kampuni  ya teknolojia za misitu yaliyojikita katika mji huu ni kampuni ya John Deere inayoongoza duniani kwa kubuni, kutengeneza na kuuza mitambo mbalimbali ya kupandia, kukata na kuvuna mazao ya misitu hususani mbao na mazao yake ili kuipa thamani sekta hiyo kuwa ya kibiashara zaidi kutokana na uzoefu wa Finland.
Ufini ambayo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia sekta ya misitu nchini Tanzania ukiwemo Mradi wa Forvac uliomalizika hivi karibuni uliochagiza ajira 500,000 katika sekta hiyo, sasa iko tayari kusaidia mradi mwingine mpya kuendeleza mageuzi hayo.
“Kutokana na uzoefu wa wenzetu katika biashara ya sekta ya misitu tayari tumekubaliana na tunakamilisha taratibu za kuanza mradi mwingine mpya ambapo Finland itaisaidia Tanzania Euro milioni 20 kuchagiza mageuzi zaidi kuifanya sekta ya misitu kuisaidia Tanzania,” aliongeza Dkt. Abbasi.
Dkt. Abbasi ameongoza ujumbe wa wataalamu ambao ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Deusdedit Bwoyo na Kamishna wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Prof. Dos Santos Silayo.
Ufini ndio nchi inayoongoza Barani Ulaya kwa kuwa na eneo lenye misitu mingi, sehemu kubwa (asilimia 60) ikimilikiwa na sekta binafsi na asilimia nyingine inayobaki ikiwa chini ya umma ikisimamiwa na kampuni binafsi ya Serikali ya Forestry LTD. Mapato ya Ufini kwa mwaka 2022 kutoka sekta ya misitu yalifikia Euro Bilioni 20 (Zaidi ya TZS Trilioni 60).

You Might Also Like

Miradi 10 Ya Kimkakati TPA Kuinua Uchumi

UDSM Yamtunuku Rais AfDB Shahada Ya Heshima Ya Sayansi

Dkt Biteko Ampongeza Mwanafunzi Aliyeelezea Miradi Ya Umeme

UDSM Yatumia Teknolojia Ya Kidijitali Kukabili Sumukuvu

Wafugaji huchakachua maziwa kwa kuongeza mafuta, maji, magadi au mkojo wa ng’ombe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wasira akipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  kwa kuenzi Falsafa za Baba wa Taifa
Next Article Rais Samia Awasili Mwanza Kilele Cha Mbio za Mwenge
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Aituza UDSM kwa Kuongoza Eneo La Elimu, Utafiti, Ubunifu Sabasaba 2025
Habari July 14, 2025
Nyanya Cheri na Ngogwe Chungu Zarejea 
Habari July 13, 2025
NFRA Yawaalika Wadau Kununua Nafaka kwa Masoko ya Ndani na Nje
Habari July 13, 2025
Kafulila: Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma Kuboresha Huduma
Habari July 13, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?