Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amesema serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha inatatua changamoto zinazowakabili vijana.
Ridhiwani amesema hayo alipomwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kufunga Kongamano la Kitaifa la Agenda ya Amani na Usalama kwa Vijana lililofanyika mkoani Dar Es Salaam.
Ametaja hatua hizo serikali ilizochukua kuwa ni ukosefu wa kazi, athari za matumizi mabaya ya teknolojia ama mitandao katika kupashana taarifa muhimu zinazowahusu vijana, uundwaji wa Baraza la Vijana na uwezeshwaji.

Ametaka vijana kuwa mabalozi wa amani na usalama, vile vile kuwa walinzi wa nchi.
