Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Mwita jijini Dar es Salaam.

Ridhiwani amesema amekutana na Mwita katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar Es Salaam.
Amesema Waziri Mwita yupo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Vijana na Amani.
