Na Lucy Lyatuu
“KAMA Kuna suala linalowasumbua wastaafu Kwa kiwango kikubwa ni utapeli pindi wanapopokea mafao yao ambapo elimu inahitajika kila mara”
Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF) amesema hayo jijini Dodoma wakati Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA),Tumaini Nyamhokya alipofanya ziara ofisini kwake Kwa ajili ya kutambulisha gazeti la MFANYAKAZI akiongozana na Mhariri Mkuu wa gazeti hilo Shani Kibwasali.
Kijazi amesema PSSSF imekuwa ikielimisha Kwa kina namna mafao yanavyotolewa na mpaka hatua ya mstaafu kuyapata lakini tatizo Bado limeendelea kuwa kubwa.
Amesema Kwa suala hilo wapo wastaafu wanaoangukia kubaki weupe kwamba wakikosa mafao yao Kwa kusikiliza matapeli ,ambapo elimu inaendelea kutolewa Ili kuokoa walio wengi .
Ni muhimu Watumishi wa Umma kuelimisha wastaafu kuwa hakuna utaratibu wowote wa malipo anayotakiwa kutoa mstaafu kwa mfuko huo ili kupata mafao yake na pindi alikutana na tatizo Hilo atoe taarifa kwa mfuko huo” amesema.
Hata hivyo amesema ni muhimu kwa wanachama wanaofika kustaafu kujiridhisha na taratibu zozote anazotakiwa Ili kuepusha hilo.
Kuhusu MFANYAKAZI,Nyamhokya ameutaka Mfuko huo kutoa taarifa na elimu mbalimbali zinazohusu wastaafu kupitia chombo hicho Ili kupanua wigo zaidi wa elimu.