Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete, amesema hivi sasa wafanyakazi wanaofanya kazi katika maeneo mawili tofauti wanaangaliwa ili waweze kuchangiwa kwenye pensheni katika maeneo yote.
Ridhiwan amesema hayo jijini Dodoma alipotembelewa na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA),Tumaini Nyamhokya aliyefika kutambulisha gazeti la MFANYAKAZI, akiongozana na Mhariri Mkuu Shani Kibwasali pamoja na waandishi wa gazeti hilo.
“Sasa hivi kwenye pensheni wale wanaofanya kazi maeneo mawili tofauti nao pia wameangaliwa katika Muswada wa Sheria Unaokuja.

“Kwa mfano madaktari unakuta anafanya kazi mbili yaani Yuko Muhimbili na akitoka anaingia Aghakan Sasa hivi kwenye skimu yetu ya pensheni kwa kuchangia ni uamuzi wako mwenyewe ukiamua wote wawili wakuchangie ni wewe, ukiamua akuchangie mmoja ni wewe,” amesema.
Amesema, ” Lakini uzuri wake upo hivi wakikuchangia waajiri wote wawili wakikuchangia ile pensheni hesabu yake inaangalia kwa ukubwa wa mchango kwa hiyo wewe ukisema usichangiwe unachangiwa na mmoja, maana yake mchango wako unakuwa mdogo. Haya ni mambo mazuri yanayofanywa na serikali.” amesema Ridhiwan Kikwete.