MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wasilisheni Migogoro Yenu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi – Massawe
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wasilisheni Migogoro Yenu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi – Massawe
Habari

Wasilisheni Migogoro Yenu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi – Massawe

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
WAFANYAKAZI walioachishwa kazi wanapaswa kuwasilisha migogoro yao Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), badala ya kuzunguka sehemu ambazo hazina mamlaka kisheria, ambapo hupoteza muda mwingi, mwisho wa siku wanakuwa nje ya muda.
Ofisa Mfawidhi CMA, Yohana Massawe amesema hayo alipozungumza na Mfanyakazi.
Amesema baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakifika katika tume hiyo kwa kuchelewa kwa kuwa walipita kwenye ofisi mbalimbali ambako sio sehemu sahihi.

“Wengine walikwenda Ofisi za Kata, wengine kwa Mjumbe, wengine kwa Waziri, au kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya lakini naomba ifahamike tu kwamba wafanyakazi wanatakiwa kutambua kwamba chombo ambacho kumeundwa rasmi kwa sheria ya Bunge ni Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa ajili ya kutatua migogoro ya kikazi.

“Kwa hiyo tunakumbushwa wafanyakazi  kutambua kuwa unapopata mgogoro unatakiwa kwenda wapi na unatakiwa kuuwasilisha ndani ya muda gani kwa migogoro ya uachishwaji ni siku 30 na migogoro mingine yote ni ndani ya siku 60 kwa hiyo tuzingatie hilo ili tusikose haki zetu za msingi kwa sababu yoyote ile,” amesema.

Amesema iwapo mfanyakazi ana sababu za msingi za kuwasilisha maombi nje ya muda ni lazima ionekane katika macho ya sheria kama ni suala la ugonjwa mfano lazima kuwe na vyeti vya hospitali.

“Kuna wale ambao wanasema walikuwa wanatibiwa kienyeji, kutibiwa kienyeji hakuna ushahidi ambao utauwasilisha kuwa ulikuwa unatibiwa kienyeji, kwa hiyo ni vizuri kufuata taratibu ambazo zipo,

“Njia ambazo ni sahihi ambazo mwisho wa siku kwenye sheria itaonekana ulikuwa na sababu za msingi, nyaraka lazima ziwasilishwe na hizo nyaraka zionyeshe wazi kuwa hukuwa na uwezo wa kuwasilisha mgogoro wako kwa sababu za ugonjwa.

“Kwa sababu unaweza ukawa unaumwa lakini bado ukawa na uwezo wa kufanya shughuli zako nyingine huku unaendelea na matibabu, huo ugonjwa lazima uwe umekufanya ushindwe kuchukua hatua ya kufungua mgogoro wako,” amesema.

Ameongeza kuwa, wengine wanachangamoto ya kuwa mahabusu uwezekano wa kufungua mgogoro ni mdogo kwa sababu mgogoro wa kikazi lazima ufunguliwe na mfanyakazi husika tofauti na migogoro mingine ya madai ambayo wakili anaweza akafungua kwa niaba.

Amesema kwenye migogoro ya kikazi mfanyakazi ni lazima ajaze ile fomu namba moja ya kuwasilisha mgogoro mbele ya tume

“Kwa hiyo sababu ya kuwa mahabusu ni sababu ya msingi lakini mara utakapotoka unatakiwa kuchukua hatua sahihi za kuwasilisha mgogoro ndani ya wakati.

“Lakini sababu nyingine inayoweza kuwa ya msingi ni iwapo mfanyakazi labda alikuwa nje ya nchi kwa sababu ambazo ni za msingi na sio kwa sababu zake binafsi.

“Kwamba ameamua kwenda kufanya maisha yake mengine lakini iwe ni kwa sababu za msingi kwamba hakuweza kuwasilisha huo mgogoro mbele ya tume ndani ya wakati,”amesema.

Amesisitiza kuwa, CMA ni chombo pekee kinachoshughulika na utatuzi wa migogoro ya kikazi.

 

You Might Also Like

JOWUTA Yakutana na Waziri Ridhiwani, Kamishna wa Kazi Kujadili Changamoto za Wanahabari

Rais Samia kufungua mkutano wa Mawaziri wa Uvuvi

SADC, Marekani Kuanzisha Jukwaa La Majadiliano

Majiko Banifu 1000 Kuuzwa Kwa Bei Ya Ruzuku Katika Maonesho Ya Madini Geita

Tanzania, Belarus Zaanza Ukurasa Mpya wa Ushirikiano wa Kimkakati

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article CMA yawataka wafanyakazi walioachishwa kazi kuwasilisha mgogoro ndani ya muda
Next Article Majaliwa Asema Sekta ya Uvuvi Yaingiza trilioni 2.9 kwa Mwaka 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Fema Mining & Drilling Mfano wa Kuigwa – Musukuma
Habari September 23, 2025
Mgodi Wa Dhahabu Wa Nyanzaga Kunufaisha Wananchi, Ujenzi Wazidi Kupaa
Habari September 23, 2025
Sekta Ya Madini Yazidi Kuchangia Ukuaji Wa Uchumi – Majaliwa
Habari September 23, 2025
Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?