MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPHPA yaonyesha ufanisi mkubwa udhibiti wa panya, kwelea kwelea
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPHPA yaonyesha ufanisi mkubwa udhibiti wa panya, kwelea kwelea
Habari

TPHPA yaonyesha ufanisi mkubwa udhibiti wa panya, kwelea kwelea

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imetunukiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kutokanana mchango wake kiuchumi na kijamii.
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa tuzo hizo kwa Taasisi zilizoonyesha juhudi katika kuwapatia jamii maendeleo endelevu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, TPHPA  imeonyesha ufanisi wa hali ya juu katika kudhibiti balaa la panya.
Taarifa inasema TPHPA imedhibiti baa la panya  katika mikoa 16, wilaya 54, kata 540, na vijiji 1,395.
“Juhudi hizi zimesaidia wakulima wapatao 58,886 kwa kuokoa jumla ya ekari 895 za mazao yao, hivyo kuimarisha usalama wa chakula na kuleta athari chanya kwa uchumi wa nchi.
“Pia TPHPA ilifanya kazi kubwa katika kudhibiti ndege aina ya kwelea kwelea. Zaidi ya ndege milioni 80 waliovamia mazao katika halmashauri 24 walikabiliwa vilivyo,” imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo udhibiti huo umewezesha wakulima kuokoa takriban tani 100,000 za nafaka, ikiwa ni pamoja na mpunga, uwele, na mtama, hivyo kuondoa hatari kubwa ya upungufu wa chakula.
Katika tukio hilo, Mamlaka iliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Profesa Andrew Temu, na Mkurugenzi Mkuu, Profesa Joseph Ndunguru, ambao walipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mamlaka.
“Tuzo hii sio tu inatambua mafanikio ya TPHPA bali pia inasisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali katika kufikia malengo ya pamoja.
“Kwa kupokea tuzo hii, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania imejidhihirisha kama mfano wa kuigwa katika juhudi za kuboresha maisha ya wananchi na kuendeleza uchumi wa nchi,” imesema taarifa hiyo.

You Might Also Like

VETA Mtwara Watua Na Mwani Maadhimishilo Ya Miaka 30

Waziri Mkuu Majaliwa Amwakilisha Dkt.Mpango Mahafali Ya 43 OUT

Fema Mining & Drilling Mfano wa Kuigwa – Musukuma

Tunatatua Malalamiko Ya Wateja – Kaguo

Ridhiwan Kikwete Apongeza Halmashauri Ya Tunduma

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Waziri Mkuu Majaliwa ndani ya SGR
Next Article Serikali Kuendelea Kuboresha Sheria za Ulinzi wa Watoto
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Habari January 9, 2026
Tuna Deni La Kusimamia Miradi Na Kusikiliza Kero za wananchi Ili Kuleta Maendeleo Ya Kweli-Salome
Habari January 9, 2026
Rais Dkt Samia Azindua Majengo Ya Kisasa
Habari January 8, 2026
TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Habari January 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?