Na Mwandishi Wetu
RAIS Samia Suluhu Hassan leo Agosti 22,2024 ameweka Jiwe la Msingi la mradi wa Ujenzi wa Suluhu Sports Academy iliyojengwa na wadau wa Maendeleo wakiongozwa na CRDB Foundation.
Katika Mradi huo kutakuwa viwanja vya michezo mbalimbali ikiwemo Uwanja wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukuwa Watazamaji 20,000.
Awamu ya kwanza ya Ujenzi wa academy hiyo inatarajiwa kukamilika Aprili mwakani.
Uwekaji wa Jiwe la Msingi ni sehemu ya Shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi festival 2024.