MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Changamoto uchakataji Mkonge kupatiwa ufumbuzi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Changamoto uchakataji Mkonge kupatiwa ufumbuzi
Habari

Changamoto uchakataji Mkonge kupatiwa ufumbuzi

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
CHANGAMOTO ya uhaba wa mashine za kuchakata Mkonge inayowakabili wakulima katika maeneo yao inatarajiwa kupatiwa ufumbuzi  utakaochochea ongezeko la uzalishaji wa zao hilo.
Hatua hiyo imetokana na ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), ambao walitembelea miradi mbalimbali ikiwamo mashamba ya Vyama vya Ushirika na Masoko (Amcos) na viwanda vya uchakataji Mkonge mkoani Tanga.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Theobald Sabi amesema pamoja na mambo mengine ziara iliyolenga kujionea Sekta ya Mkonge kuanzia kwenye mashamba hadi uchakataji na kuelewa kwa ujumla mnyororo mzima wa thamani wa sekta hiyo lakini pia changamoto zinazowakabili wakulima na wote waliopo kwenye sekta ndogo ya Mkonge.
“Nia yetu ni kuhakikisha kwamba tunapata suluhisho la changamoto ambazo zimekuwapo hasa kwenye eneo la uchakataji mkonge.
“Tumejionea mashine ambazo zinafanya vizuri na zile zenye changamoto tutachukua hatua kama bodi kuhakikisha kwamba shughuli nzima za Mkonge zinakwenda vizuri ili tujenge tija kwa wakulima, mamlaka, bodi, uchumi na pato la taifa kwa ujumla,” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TSB, Saddy Kambona amesema licha ya ziara hiyo ya kujifunza na kujenga uelewa lakini jambo kubwa ambalo walitaka kujionea ni kukosekana kwa mitambo ya uchakataji Mkonge na kupata jawabu kwa wakulima juu ya namna ya kuondokana na changamoto hiyo.
“Kwa hiyo tuliwapitisha maeneo mbalimbali lakini pia tukawaonesha jitihada ambazo sisi kama bodi au menejimenti tumezichukua kuondoa hiyo changamoto ya uchakataji ukiondoa jitihada ambazo tunaendelea nazo kupitia wizara yetu ya kilimo ya mipango ya serikali kununua mitambo ya uchakataji na kuiweka maeneo mbalimbali.
“Lakini pia tuchukue nafasi nyingine kuwakaribisha wawekezaji binafsi kuwekeza mitambo kwenye mashamba hapa Korogwe ili kujaribu kupunguza changamoto za uchakataji ambazo zimekuwa zikilalamikiwa mara kwa mara.
“Leo wakurugenzi wamejionea tofauti iliyopo kati ya mitambo ambayo imekuwepo miaka yote ambayo imekuwa ikiendeshwa na Sisalana lakini na ile mitambo mipya ambayo imewekezwa na wawekezaji binafsi ikiwamo Hale na Magunga hatua hiyo imesaidia kupunguza changamoto ya uchakataji kwa wakulima katika maeneo yao,” amesema.
Aidha, amesema Menejimenti inategemea baada ya ziara hiyo watakapokutana kwenye kikao cha bodi watapokea maelekezo mbalimbali baada ya wakurugenzi kujionea hali halisi kwenye hizo Amcos na uchakataji unavyokwenda.
Naye Mjumbe wa Bodi hiyo, Naweed Mullah, amesema katika ziara hiyo wamejionea mazuri mengi ambapo ametoa wito bodi kuangalia namna watu wa uchakataji waongezeke lakini pia waangalie namna ya kutoa huduma ili kuwe na bei nafuu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Magunga Amcos na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Amcos za Mkonge Tanga, Shedrack Lugendo aliishukuru bodi kuwatembelea na kujionea shughuli wanazofanya na kuongeza kuwa mitambo ya uchakataji Mkonge ya Kampuni ya Sisalana imepitwa na wakati na hazina matengenezo mazuri ambapo mkonge mwingi unaishia kwenye mtaro mkulima anapata hasara.

You Might Also Like

Apongeza watumishi kwa kutoa huduma bora kwa walimu

Uongozi CHADEMA Kanda Ya Kati Upo Imara

BMT Yaleta Kicheko Kwenye Michezo

Wahitimu Kidato IV 2024, Washauriwa Kubadili Machaguo Ya Tahasusi

Wasilisheni Migogoro Yenu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi – Massawe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Watanzania wasisitizwa kulinda mazingira ya miundombinu ya umeme
Next Article Waziri Jenista akabidhiwa ofisi rasmi na Ummy Mwalimu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?