Na Lucy Ngowi
DODOMA: Ofisa Masoko wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania, Halima Tosiri amekaribisha wawekezaji katika maeneo ya hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu kuwekeza katika maeneo tengefu.
Amesema wawekezaji wanakaribishwa katika maeneo yote vwanaofanya shughuli za utalii kwa kuwelekeza migahawa ambayo inaendana na uhifadhi,michezo na mambo mengine.
Pia Halima ametoa wito kwa watanzania kutembelea hifadhi hizo kwa ajili ya kushuhudia uzuri na rasilimali za bagari ambazo zipo Tanzania.