Na Lucy Ngowi
DODOMA: MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imejipanga kutatua kero za kikodi kwa wananchi waliokutana na changamoto mbalimbali.
Kamishna Mkuu wa TRA. Yusuph Juma Mwenda amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na wavuvi yanayoendelea Jijini Dodoma.
Mwenda amesema, ” ili eneo ni moja ya eneo ambalo tutachukua changamoto za kikodi za walipa kodi na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.
“Kwa hiyo nitoe wito wale wananchi wenye changamoto waje waonane na watu wetu waeleze wanachokihitaji wapate elimu,” amesema.
Pia amesema katika maonesho hayo TRA imejipanga kuhudumia walipa kodi kwa haraka kwenye maeneo mbalimbali wanayohitaji ili kuyapatia ufumbuzi waweze kuchangia kodi.
Awali aliwataka watanzania waliofikia kiwango cha kulipa kodi , wafike katika banda la TRA kwenye maonesho hayo ili wapate elimu ya kodi, mabadiliko ya sheria na pia ikiwa ni pamoja huduma za kuwakadiria kiasi wanachopaswa kukilipia kutokana na biashara wanazozifanya.
Alisisitiza kuwa, kiongozi bora ni yule anayofanya yale anayopaswa kuyafanya na kumtolea mfano Rais Samia Suluhu Hassan kuwa anapaswa kuigwa yale anayoyafanya katika nchi kwa uadilifu.
“Kiongozi bora ni yule anayofanyq yale aliyoahidi kuyafanya. Kwa mfano kwa wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati.
“Rais Samia anachokifanya cha kodi zinazotolewa na wananchi, anazitumia vizuri katika kuliletea taifa maendeleo kwa mfano kujengea barabara, kuboreshea elimu katika maeneo tofauti, huduma za afya na maeneo mengine,” amesema.