Na Lucy Lyatuu
Dar es Salaam: SERIKALI inatarajia kuzindua sera mpya ya Taifa ya Biashara yenye dhamira ya kuweka mfumo na mkakati madhubuti unaolenga kuboresha mazingira ya biashara,kuongeza ukuaji wa kiuchumi na kuboresha ustawi wa wananchi.
Sera hiyo ni marejeo ya sera ya mwaka 2003 ambayo imefanyiwa marekebisho Ili iweze kuendana na mabadiliko ambayo yametokea katika nyanja mbalimbali kikanda na Kimataifa.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amesema hayo Dar es Salaam na kuongeza kuwa Naibu Waziri Mkuu Dkt.Dotto Biteko atazindua sera hiyo kesho.
Amesema sera hiyo inaongozwa na kauli mbiu isemayo ushindani wa biashara katika kuchochea kasi ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi yanayoongozwa na viwanda.
Amesema hafla ya uzimduzi huo inajumuisha wadau mbalimbali wapatao 300 kutoka taasisi za umma,taasisi Binafsi,mashirika ya dini,wabia wa maendeleo,mabalozi,vyama vya wafanyabiashara na wenye viwanda na wafanyabiashara.
Dk Jafo amesema sera hiyo itaimarisha, kuku,a na kuendeleza biashara ya ndani na nje,kuimarisha mtangano na ushiriki wa nchi katika biashara na nchi zingine rafiki za kikanda na Kimataifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark Afrika,Elibariki Shami amesema ni sera itakayoleta uratibu wa biashara baina taasisi na taasisi