Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kulinda taswira nzuri ya Wakala huo.
Rai hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA. Victor Seff wakati akizungumza na watumishi wa TARURA mkoa wa Kigoma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa.
Seff amesema kufanya kazi kwa bidii ni msingi wa kutekeleza majukumu ya Wakala na kuleta tija katika malengo na kukamilisha ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa ufanisi mkubwa.
Pia Seff alitembelea na kukagua barabara za Manispaa ya Kigoma -Ujiji na kumwagiza Meneja wa TARURA Mkoa kuhakikisha wanazifanyia matengenezo ya mara kwa mara barabara zilizojengwa ili kuzilinda na kuzifanya zidumu kwa muda mrefu.