Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 4

TEA Yapitia Mpango Mpya Wa Miaka Mitano

Na Mwandishi Wetu
MOROGORO: MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeanza hatua za kuandaa mwelekeo mpya wa utekelezaji wa majukumu yake kwa miaka mitano ijayo, baada ya Baraza la Wafanyakazi kujadili Mpango Mkakati wa Tano wa 2026/27–2030/31.
Katika kikao hicho, wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi pia wametathmini utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Nne wa 2021/22–2025/26 ili kubaini mafanikio yaliyopatikana na maeneo yanayohitaji kuimarishwa.
Akizungumza katika Kikao cha Pili cha Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa TEA, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Erasmus Kipesha, amesisitiza umuhimu wa wajumbe kutoa maoni na kushiriki kikamilifu katika kuboresha mpango huo.
Amesema ushiriki wa wafanyakazi ni muhimu katika kuhakikisha mpango unaoandaliwa unaakisi vipaumbele vya Mamlaka na kuwezesha utekelezaji wa majukumu yake kwa ufanisi.
Habari Picha 14276
Mpango Mkakati wa Tano umezingatia miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2023 pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Katika kikao hicho kilichofanyika Morogoro Novemba 2 na 3, 2026, wajumbe pia walijadili taarifa ya mapitio ya Sheria ya Mfuko wa Elimu ya mwaka 2001, hatua inayolenga kuimarisha utendaji na ufanisi wa Mamlaka hiyo.
Habari Picha 14277
Habari Picha 14278
Habari Picha 14279
Habari Picha 14280
Habari Picha 14281
Habari Picha 14282
Habari Picha 14283
Habari Picha 14284
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.