Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 6

TEA, UNICEF Wajenga Vyoo 23 Mtangani

Wanafunzi zaidi ya 310 kunufaika na mradi wa Sh. Milioni 144.8

Na Mwandishi Wetu

PEMBA: WANAFUNZI zaidi ya 310 wa Shule ya Sekondari Mtangani, Wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba, wanatarajia kunufaika na matundu 23 ya vyoo yaliyojengwa kwa gharama ya Sh. Milioni 144.8, kwa ufadhili wa Serikali ya Canada kupitia Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), kwa ushirikiano na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Ujenzi huo unalenga kuondoa changamoto ya ukosefu wa vyoo iliyokuwa ikiikabili shule hiyo, ambapo walimu na wanafunzi walilazimika kutumia vyoo vya shule ya msingi iliyopo umbali wa takribani mita 150.

Habari Picha 14230

Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi TEA  Mwanahamis Chambega akikagua ujenzi wa Shule ya Amali ya Kangagani Wilaya Wete Pemba

Akizungumza wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, Mwanahamis Chambega, mwakilishi wa Msimamizi Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohamed Hassan Ally, amesema hali hiyo ilikuwa ikiathiri afya, usalama na mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Amesema ukosefu wa vyoo pia ulichangia utoro na kuathiri maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi.

Ally ameishukuru TEA, UNICEF na Serikali ya Canada kwa kufanikisha mradi huo, akieleza kuwa utaboresha mahudhurio na mazingira ya shule.

Kwa upande wake, Chambega amesema ameridhishwa na ubora wa ujenzi huo, huku akiwataka walimu, wanafunzi na viongozi wa shule kutunza miundombinu hiyo ili idumu kwa muda mrefu.

Katika ziara hiyo, amekagua pia ujenzi wa Shule ya Amali ya Kangagani, Wete, na ukarabati wa maabara za sayansi katika shule za sekondari Piki na Kangani.

Habari Picha 14228

Muonekano wa nje wa matundu ya vyoo katika shule ya Sekondari Mtangani iliyopo Wilaya ya Mkoani Pemba

TEA na UNICEF zinashirikiana kutekeleza miradi 20 ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu Zanzibar, ikiwamo miradi 15 ya awamu ya kwanza inayolenga kuboresha masomo ya Sayansi, Hisabati na Teknolojia (STEM).

Habari Picha 14231

Moja ya choo cha watu wenye mahitaji maalumu Shule ya Sekondari Mtangani Wilaya ya Mkoani Pemba

Habari Picha 14234

Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi TEA  Mwanahamis Chambega akikagua ukarabati wa maabara ya Sayansi Shule ya Sekondari Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba

 

Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.