Na Lucy Lyatuu,Tanga
MKUU wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Ayubu Sebabile amewaeleza wanafunzi wa shule za sekondari mkoani humo kuwa wana nafasi kubwa ya kuja na bunifu unaoweza kusaidia eneo la chakula na lishe na kuiwezesha nchi kufikia malengo.
Amesema hayo katika shindano maalum la ubunifu kwa wanafunzi 32 wa shule za sekondari mkoani humo lililoratibiwa na Shirika la Kilimo Na Chakula Duniani (FAO) likifanyika katika siku ya chakula duniani inayoadhimishwa mkoani humo.
Katika shindano hilo wanafunzi hao wanatakiwa kuja na ubunifu wa kuchora namna nchini inavyoweza kuimarisha chakula na lishe jambo litakaloibua vipaji vyao.

Akizungumza Sebabile aliwataka wanafunzi hao kutambua kuwa chakula ndio nishati ya mwili na kwamba kwa kutumia fursa hiyo wanayo nafasi kubwa ya kuja na ubunifu unaoleta chachu katika eneo la chakula.
Amesema katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya maendeleo 2050 nchi inakusudia kuwa mzalishaji namba moja kwa chakula Afrika na kwamba ni.muhimu wanafunzi wakaja na ubunifu utakaowezesha kufikia malengo ya uzslishaji wa chakula.
Kwa upande wake Mwakilishi Msaidizi wa FAO nchini, Charles Tulahi amesema wanafunzi hao wanatoka shule za sekondari ya Mwapachu,Kiomoni, Pagala na UmmyMwalimu.
Amesema wataonesha ubunifu wao utakaowezesha kutambua vipaji walivyo navyo kwa kuwa wana mchango mkubwa katika eneo la chakula na lishe.
Amesema kupitia shindano hilo kutakuza vipaji vyao wao na kuwekeza na kuwekeza zaidi kwenye ubunifu.
Maoni 0
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!