Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 12

NFRA Yafundisha  Wakulima Mbinu Za Kuhifadhi Mazao

Na Lucy Lyatuu,Tanga

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi Ya Chakula (NFRA)  inaelimisha jamii mbinu mbalimbali za uhifadhi wa  chakula ili wakulima waweze kutunza chakula kwa njia zilizo bora pamoja na kukabiliana na mvua za Elnino.

Ofisa Kilimo kuyoka NFRA Mathay Hhando amesema hayo katika siku ya chakula duniani inayoadhimishwa mkoani Tanga katika viwanja vya Usagara.
Amesema NFRA inawafundisha wakulima kuhifadhi chakula kwa mbinu bora ili kisiharibike na kuwa salama kwa matumizi.
Habari Picha 14119
Amesema mkulima anaweza kuhifadhi chakula kwenye mifuko maalum lakini sharti isiwekwe kugusana na sakafu ama ukuta wa nyumba kuepusha unyevunyevu pamoja na wadudu kama panya ,jambo litakalowezesha nafaka kukaa kwa  muda mrefu huku akiepuka pia kutumia  viuatilifu kuhifadhi mazao.
“Matumizi ya viuatilifu ni gharama na kwa kutumia njia ya asili mkulima anaweza pia kuhifadhi  mazao katika kihenge cha bati maalum pale ambapo mazao yanakuwa yamekauka,” amesema.
Akizungumzia  matumizi ya chumvi na chupa  katika kutambua kama nafaka imekauka amesema mkulima ataweka robo ya mazao hayo kwenye chupa ya plastiki ambayo ni kavu na kuchanganya  na vijiko viwili vya  chumvi na kutikisa.
Habari Picha 14120
Amesema baada ya hagua hiyo anaiweka chupa hiyo kwenye kivuli na baada ya dakika tano kama chumvi ndani ya  chupa itaonesha kuyeyuka ni wazi kuwa mazao hayajakauka ipasavyo.
Amesema iwapo chumvi haitoyeyuka na kubakia kama ilivyo basi mazao hayo yanakuwanyamekauka na yanahitaji kuhifadhiwa.
“Zipo njia nyingine za kujua kama mazao yamekauka ikiwa ni pamoja na kung’ata punje,kusikiliza mlio wa mazao kwa kumimina kwenye vyombo,” amesema na kuongeza kuwa njia nyingine ya kisasa ninkutumia mashine maalum yankupima unyevu kwenye mazao.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.