Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 9

Chai Ina Faida Nyingi, Wananchi Wahamasishwa Kuitumia Mara Nyingi

Na Lucy Lyatuu,Tanga

BODI Ya Chai Tanzania inawahamasisha wananchi kunywa chai kwa wingi kwa kuwa ninkinywahi bora chenye faida kubwa kutokana na  viini lishe vilivyomo ndani yake.
Ofisa Mkaguzi kwenye Bodi hiyo Kanda ya Kaskazini Jilala sitta amesema hayo wakati akizungumza katika wiki ya chakula duniani inayoadhimishwa mkoani Tanga katika viwanja vya Usagara.
Amesema wananchi wanapaswa kufahamu faida zilizopo katika chai kwamba madininya calsium yaliyopo husaidia kuimarisha mfumo wa moyo na kuuganya kuwa imara katika kusukuma damu mwilini na kuimarisha  mishipa ya damu.
Amesema ina kiambata cha kuyeyusha mafuta yasiyofaaa ndani ya mwili na pia husaidia mmeng’enyo wa chakula na kusaidia kuleta naguu kwa kuuanya mwili kuwa mwepesi na kuondoa msongo wa mawazo.
Sitta amesema madininya fluoride  yaliyopo ndanibya chai husaidia kuboresha afya ya kinywa,hivyo ni muhimu jamii kunywa chai mara kwa ili kunufaika.
“Chai haina madhara yoyote bali ina faida zaidi kwa mtumiaji na inasisitizwa kutumia chai muda wowote hata bila kuweka sukari,” amesema na kuongeza kuwa  wananchi  kuzijua pia fursa za kuwekeza kwenye chai kwa kulima,kusindika na hata  kuzitumia teknolojiabza uzalishaji chai.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.