Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 17

GF TRUCKS YAFUNGUA SOKO GEITA

Yakabidhi Magari Kwa Wateja
Na Lucy Ngowi
GEITA: MAONESHO ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yameanza kuzaa matokeo ya moja kwa moja ya kibiashara baada ya kampuni ya GF Trucks & Equipment kukabidhi magari kwa wateja wake, hatua inayoonyesha namna jukwaa hilo linavyogeuka kuwa soko la kuunganisha mahitaji ya wachimbaji na watoa huduma.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Geita, ambako kampuni hiyo imeshiriki kuonesha magari na vifaa vinavyoweza kutumika katika shughuli za uchimbaji madini na shughuli nyingine za kiuchumi.
Habari Picha 13973
Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja Biashara na Masoko wa GF Trucks & Equipment, Smart Deus, amesema kampuni hiyo imetumia maonesho hayo kukutana moja kwa moja na wateja, kutangaza bidhaa na huduma zake pamoja na kukabidhi magari yaliyonunuliwa na wateja.
Amesema uwepo wa kampuni hiyo katika maonesho hayo unaipa fursa ya kuwafikia wadau wa madini, hususan wachimbaji na kampuni zinazotoa huduma migodini, ambao wanahitaji magari na vifaa vya kuendeshea shughuli zao.
“Maonesho haya yametupa nafasi ya kukutana na wateja, kuonesha bidhaa zetu na pia kukabidhi magari ambayo yamenunuliwa,” amesema Deus.
Habari Picha 13974
Ameongeza kuwa GF Trucks & Equipment pia ina kiwanda cha kuunganisha magari, GF Vehicle Assemblers, kilichopo Kibaha mkoani Pwani, kinachoshiriki katika mnyororo wa thamani wa sekta ya magari nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Amotech Mine Services, Joffrey Mwaselera, amesema kampuni yake imepokea gari aina ya Mahindra alilolinunua kupitia GF Trucks & Equipment wakati wa maonesho hayo.
Mwaselera amesema kampuni yake inayotoa huduma za uchimbaji madini, ikiwemo uchorongaji, usafirishaji na uchimbaji, inahitaji magari na vifaa vinavyoweza kuongeza ufanisi wa shughuli zake.
Amesema ushirikiano huo kati ya Amotech Mine Services na GF Trucks & Equipment unaonyesha umuhimu wa kuwaunganisha watoa huduma za madini na kampuni zinazozalisha au kusambaza vifaa vinavyohitajika katika migodi.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.