Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 17

NABII ELIYA: Mafanikio Yetu Ni Kumwinua Mchimbaji Mdogo

Na Licy Ngowi
GEITA: KAMPUNI ya Nabii Eliya imesema mafanikio yake katika sekta ya madini hayapimwi kwa faida pekee, bali pia kwa uwezo wake wa kuwainua wachimbaji wadogo kwa kuwapatia teknolojia na huduma za kiufundi zinazoongeza tija na usalama katika shughuli zao.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Nabii Makuri
amesema hayo wakati wa siku maalumu ya Wachimbaji Wadogo na Watoaji wa Msaada wa Kiufundi (TSA), katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Geita.
Habari Picha 13842
Amesema kwa muda mrefu wachimbaji wadogo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo uzalishaji mdogo, gharama kubwa za uendeshaji na ukosefu wa usalama katika maeneo ya kazi.
Amesema kampuni yake imeamua kukabiliana na changamoto hizo kwa kutoa huduma za kiufundi na teknolojia zinazolenga kuongeza uzalishaji, kupunguza gharama na kuimarisha usalama wa wachimbaji.
“Lengo letu si biashara tu, ni kuinua mchimbaji mdogo. Tunapompa mchimbaji teknolojia sahihi, tunampa matumaini ya kesho iliyo bora kwa familia yake na jamii yake,” amesema.
Amefafanua kuwa hatua nyingine wanazochukua ni kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata ajira na ujuzi wa vitendo kupitia shughuli za migodini, huku wakihamasisha matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira na yenye gharama nafuu.
Amesema kampuni hiyo pia imedhamiria kurejesha sehemu ya manufaa ya shughuli zake kwa jamii kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii.
Maonesho hayo yanafanyika chini ya kaulimbiu “Kuwezesha Wachimbaji Wadogo, Kuongeza Tija, Kujenga Sekta Imara”, yakilenga kutoa fursa kwa wadau wa madini kujifunza na kuonesha teknolojia zinazoweza kuongeza ufanisi katika shughuli za uchimbaji.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.