MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yaendelea Kuchukua Hatua Kuimarisha Sekta Ya Elimu,Kupanua Fursa Za Elimu Ya Sekondari
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yaendelea Kuchukua Hatua Kuimarisha Sekta Ya Elimu,Kupanua Fursa Za Elimu Ya Sekondari
Habari

Serikali Yaendelea Kuchukua Hatua Kuimarisha Sekta Ya Elimu,Kupanua Fursa Za Elimu Ya Sekondari

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI  imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta ya elimu kwa kuongeza miaka ya elimu ya lazima, kupanua fursa za elimu ya sekondari na kuimarisha mafunzo ya ufundi ili kuwapa vijana uwezo wa kushiriki kikamilifu katika soko la ajira.
Akizungumza Septemba  jijini Dodoma na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema maandalizi ya utekelezaji wa miaka 10 ya elimu ya lazima kuanzia mwaka 2028 yanaendelea, hatua itakayohitaji miundombinu, walimu na nafasi za kutosha katika shule za sekondari.
Profesa Mkenda amebainisha kuwa mpango huo utasababisha ongezeko kubwa la wanafunzi watakaoingia sekondari, hivyo Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili wanapata nafasi ya kuendelea na masomo.
Habari Picha 13573
Aidha, ameongeza kuwa  Serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa elimu wenye mikondo ya elimu ya jumla na elimu ya amali, ili wanafunzi wapate maarifa na stadi zinazowawezesha kuajirika au kujiajiri.
Katika mazungumzo hayo, Profesa Mkenda ameeleza kuwa Serikali inajenga vyuo vya ufundi katika maeneo mbalimbali na kuimarisha mafunzo ya ufundi ili kukidhi mahitaji ya vijana na uchumi wa Taifa.
Profesa Mkenda ameongeza kuwa Serikali inawekeza katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati pamoja na teknolojia mpya kama akili bandia (AI), ujifunzaji wa mashine na usalama wa mtandao, ili kuandaa wataalamu wa kisasa.
Habari Picha 13574
Amesisitiza  umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi katika kupanua fursa za elimu, hususan katika ujenzi wa miundombinu na utoaji wa elimu ya amali.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Carolyne Nombo, amesema kuwa Serikali inatazama uwezekano wa kuboresha vivutio vya kisera vitakavyoongeza uwekezaji wa sekta binafsi katika elimu.
Habari Picha 13575
Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Marianne Young, amepongeza juhudi za Tanzania na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika elimu na na mafunzo ya  ufundi, ikiwemo kuunganisha taasisi za Tanzania na vyuo vikuu vya Uingereza katika maeneo ya teknolojia ya kisasa na mazingira.
Habari Picha 13576
Habari Picha 13577

You Might Also Like

Serikali Kuendelea Kutenga Fedha Kwa ajili ya Ukamilishaji wa Maboma ya Vituo vya Afya

Kamati Ya Bunge Yapongeza Usimikaji Mfumo Wa Kidijitali CMA

Biteko Atoa Somo Uzalishaji Matumizi ya NIishati Afrika

Ndoinyo Aishauri Serikali Kurejesha Utalii Vijijini

Serikali Yawapeleka Wauguzi 101 Nchini Saudi Arabia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yachunguza Sheria Mpya Ya Biashara Mtandao
Next Article Ujenzi Sports Club Yatoa Msaada Kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Dodoma
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ujenzi Sports Club Yatoa Msaada Kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Dodoma
Habari September 3, 2026
Serikali Yachunguza Sheria Mpya Ya Biashara Mtandao
Habari September 3, 2026
Zhou Enlai na Julius Nyerere: Urafiki Uliovuka Mipaka Milima, Bahari
Makala September 2, 2026
TANESCO Yabaini Matukio Ya Wizi Wa Umeme Kinondoni Kaskazini
Habari September 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?