MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TANESCO Yabaini Matukio Ya Wizi Wa Umeme Kinondoni Kaskazini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TANESCO Yabaini Matukio Ya Wizi Wa Umeme Kinondoni Kaskazini
Habari

TANESCO Yabaini Matukio Ya Wizi Wa Umeme Kinondoni Kaskazini

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA  la Umeme Tanzania (TANESCO) limebaini matukio ya wizi wa umeme katika eneo la Visiwani, Mwananyamala na Mivumoni, zilizo Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, wakati wa operesheni ya ukaguzi wa mita na miundombinu ya umeme inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
Operesheni hiyo inalenga kudhibiti matumizi yasiyo halali ya umeme, kulinda miundombinu ya Shirika na kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kutolewa kwa usalama na ufanisi kwa wananchi.
Habari Picha 13551
Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, Afisa Usalama wa TANESCO,  Lilian Nizim, amewataka wananchi kuzingatia sheria na taratibu za matumizi ya umeme na kuepuka vitendo vya kuingilia au kuchezea mita za umeme.
“Mteja anapobaini changamoto yoyote inayohusiana na mita yake, anapaswa kutoa taarifa TANESCO ili ipatiwe ufumbuzi. Ni muhimu wananchi waepuke kabisa kuingilia mita kwa njia yoyote, kwani ni kinyume cha sheria na kunaweza kuhatarisha usalama wa maisha na mali,” amesema  Nizim.
Habari Picha 13552
Kwa upande wake, Mhandisi wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kaskazini,  Underson Manyika, amesema wakati wa ukaguzi katika eneo la Visiwani, timu ya wataalamu ilibaini baadhi ya wateja wakiwa wamechepusha nyaya za umeme, hali iliyosababisha mita kutosoma matumizi halisi ya umeme.
“Ukaguzi wetu umebaini kuwepo kwa miunganisho isiyo halali iliyokuwa ikiathiri usomaji sahihi wa mita. Hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Shirika,” amesema  Manyika.
Habari Picha 13553
Amesema vitendo vya wizi wa umeme husababisha hasara kwa Shirika, kuhatarisha usalama wa wananchi na kuathiri ubora wa huduma ya umeme, hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na TANESCO kwa kutoa taarifa za vitendo hivyo ili viweze kudhibitiwa kwa wakati.
TANESCO inaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mita na miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha utoaji wa huduma ya umeme ya uhakika, salama na endelevu kwa wananchi.
Habari Picha 13554

You Might Also Like

Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza

PURA Yajivunia Agenda Ya Matumizi Ya Nishati Safi

Dkt Natu Mwamba Ashuhudia Utiaji Saini CRDB Na Taasisi Tatu Za Fedha Kimataifa

Chalamila Akabidhi milioni 100, saruji Kukamilisha Zahanati

Mkenda: Maendeleo ya Taifa Yanategemea Sayansi na Teknolojia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article MOI Yafanikiwa Kupunguza Rufaa Za  Wagonjwa Wa Mifupa Kwa Asilimia 98
Next Article Zhou Enlai na Julius Nyerere: Urafiki Uliovuka Mipaka Milima, Bahari
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Zhou Enlai na Julius Nyerere: Urafiki Uliovuka Mipaka Milima, Bahari
Makala September 2, 2026
MOI Yafanikiwa Kupunguza Rufaa Za  Wagonjwa Wa Mifupa Kwa Asilimia 98
Habari September 1, 2026
Sera Ya Ardhi Inatoa Fursa Kwa  Wanawake Kumiliki Ardhi
Habari August 31, 2026
Walimu 600 Washindanishwa Kutumia AI Darasani
Habari August 30, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?