MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku
Makala

Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
5 Min Read
Na Lucy Ngowi
MIAKA 40 ya maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu nchini imeendelea kuzaa matokeo chanya, huku wabunifu wakitumia maarifa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, wakiwamo wafugaji wa kuku.
Miongoni mwao ni Nemo Swalehe, mfugaji na mjasiriamali kutoka Mbeya, ambaye amebuni dawa ya kusafisha mayai kwa lengo la kupunguza uwezekano wa mayai kuharibika wakati wa uanguaji.
Nemo, ambaye amehitimu katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), anasema wazo la ubunifu huo lilitokana na changamoto aliyokutana nayo katika shughuli za ufugaji wa kuku, hasa upotevu wa mayai wakati wa uanguaji.
Anasema changamoto hiyo iliongezeka mwaka 2023 na kuendelea, hali iliyomsukuma kutafuta suluhisho litakalowasaidia wafugaji kupunguza hasara.
Kwa mujibu wa Nemo, mwaka 2025 alipokuwa darasani, alijifunza kuhusu muundo wa yai na kugundua kuwa yai lina matundu madogo yanayowezesha kubadilishana hewa.
Anasema kupitia matundu hayo, bakteria na fangasi wanaweza kupata nafasi ya kuingia ndani ya yai na kusababisha kuharibika, jambo linaloweza kupunguza kiwango cha mayai yanayofanikiwa kuanguliwa.
Habari Picha 13382
“Ndipo tulipoanza kutafuta namna ya kuua vijidudu hivyo kabla ya mayai kuwekwa kwenye mashine ya kuatamia. Tukaja na dawa ambayo inanyunyizwa kwenye mayai ili kuua vijidudu,” anasema.
Nemo anasema dawa hiyo imeundwa kuwa rahisi na salama kwa matumizi ya wafugaji wadogo, tofauti na baadhi ya njia zinazotumiwa na wafugaji wakubwa ambazo zinahitaji maandalizi maalumu na utaalamu katika matumizi yake.
Anasema dawa hiyo inaonekana kama maji, haina harufu na imekusudiwa kutumiwa kwa kunyunyizia mayai kabla ya kuwekwa kwenye mashine ya kuatamia.
“Lengo letu ni kupata kitu ambacho ni salama na ambacho mfugaji yeyote anaweza kutumia. Hata mama mwenye kuku wachache nyumbani anaweza kutumia dawa hii,” anasema.
Anafafanua kuwa dawa hiyo haiwezi kuhakikisha kila yai litaanguliwa, bali kazi yake kubwa ni kupunguza au kuua vijidudu vinavyoweza kusababisha yai kuharibika.
Kwa mfugaji anayefanya uanguaji wa vifaranga, bunifu hiyo inaweza kuwa na umuhimu katika kupunguza hasara zinazotokana na mayai kuharibika kabla ya kuanguliwa, hivyo kuongeza ufanisi wa uzalishaji endapo itathibitishwa na kufikia hatua ya kutumika kibiashara.
Nemo anasema katika safari ya kuendeleza ubunifu huo, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imekuwa miongoni mwa taasisi zilizompa msukumo na kumfungulia fursa ya kuendeleza kazi yake.
Anasema amepata nafasi ya kushiriki katika shughuli za COSTECH na kuwa mmoja wa washindi wa programu za ubunifu, hatua iliyomwezesha kupata msaada wa kifedha kwa ajili ya kuendeleza bunifu hiyo.
“Nashukuru COSTECH kwa sababu imenitia moyo sana. Kutoka nilipoanza hadi kufikia hapa, nimepata msaada na sasa nimepata mkono wa Serikali kupitia COSTECH ambao utanisaidia kusonga mbele na kufikia wafugaji wengi zaidi nchini,” anasema.
Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo, Dkt. Amos Nungu, anasema Serikali kupitia COSTECH inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana wenye ubunifu, kuwaunganisha na taasisi mbalimbali na kuwawezesha kupata mitaji ili bunifu zao zifikie hatua ya kibiashara.
Dkt. Nungu pia anasisitiza umuhimu wa vijana kutumia fursa zinazotolewa na taasisi mbalimbali kukuza vipaji, ujuzi na bunifu zao, badala ya kusubiri fursa ziwafuate.
Kwa Nemo, msaada huo ni sehemu ya safari ya kubadilisha wazo lililoanzia kwenye changamoto ya mfugaji kuwa bidhaa inayoweza kuwafikia wafugaji wengi zaidi.
Anasema msaada huo utamwezesha kuendeleza bidhaa hiyo na hatimaye kuifikisha kwa wafugaji katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Hata hivyo, anasema dawa hiyo bado haijaanza kupatikana katika maduka kwa ajili ya matumizi ya jumla, akieleza kuwa kazi inaendelea kuhakikisha inafikia hatua ya kupatikana kwa urahisi kwa walengwa.
Bunifu hiyo ni miongoni mwa mifano inayoonesha namna uwekezaji katika sayansi, teknolojia na ubunifu unavyoweza kubadili changamoto za kila siku kuwa fursa za kiuchumi na kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji.
Katika maadhimisho ya miaka 40 ya COSTECH, simulizi ya Nemo inaonesha safari ya bunifu kutoka kwenye changamoto ya mfugaji, darasani, hadi kupata msaada wa taasisi unaoweza kuifikisha katika hatua ya uzalishaji na matumizi mapana.
Habari Picha 13381
Kwa kuendelea kuungwa mkono na taasisi za utafiti, elimu na uwezeshaji, bunifu kama hiyo inaweza kuwa sehemu ya suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wafugaji na wakati huo huo kufungua fursa mpya za biashara kwa vijana wabunifu.
Nemo anasema anaamini kwa kuendelea kupata ushirikiano, bunifu hiyo inaweza kuwafikia wafugaji wengi zaidi na kusaidia kupunguza hasara zinazotokana na kuharibika kwa mayai wakati wa uanguaji.

You Might Also Like

Miaka 40 ya Costech: Ruzuku ya Ubunifu Imegeuza Wazo Kuwa Kiwanda Cha Kimataifa

Ushirikiano Wa Afrika, China Kuonyesha Mwelekeo Maendeleo Ya Dunia

Kitabu cha Utamaduni na Maendeleo Nchini Tanzania, Chaimarisha Mawasiliano ya Kitamaduni Baina ya China, Tanzania

Kinywaji Cha China Chavuka Mipaka Chatua Tanzania

Barabara Zinazopasuka, Suluhisho Linalotoka Maabara za Tanzania

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Habari August 22, 2026
Maji Yageuka Gesi, Lusano Aibua Ubunifu wa Nishati Safi
Makala August 22, 2026
Bunifu Ya Dawa Ya Mayai Kupunguza Hasara Kwa Wafugaji Wa Kuku
Makala August 22, 2026
TTCL Yazindua Awamu Ya Pili,’Faiba Mlangoni Kwako’ Yasisitiza Kupanua Wigo Wa Huduma
Habari August 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?