MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TTCL Yazindua Awamu Ya Pili,’Faiba Mlangoni Kwako’ Yasisitiza Kupanua Wigo Wa Huduma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TTCL Yazindua Awamu Ya Pili,’Faiba Mlangoni Kwako’ Yasisitiza Kupanua Wigo Wa Huduma
Habari

TTCL Yazindua Awamu Ya Pili,’Faiba Mlangoni Kwako’ Yasisitiza Kupanua Wigo Wa Huduma

Author
By Author
Share
5 Min Read
Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam
SERIKALI imelitaka Shirika La Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema limejipanga vyema kupanua wigo wa huduma ya faiba kwa kuhakikisha inafika katika maeneo yenye makazi yanayokua, masoko, maeneo ya biashara, viwanda, shule, vyuo, vituo vya afya na ofisi za Serikali Tanzania Bara na Zanzibar.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah   Kairuki, amesema hayo  Dar es Salaam wakati akizindua rasmi utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mradi  na kusisitiza kuwa mafanikio ya mradi hayapaswi kupimwa kwa idadi ya miundombinu iliyojengwa pekee, bali kwa idadi ya wateja wanaounganishwa, ubora wa huduma, kasi ya intaneti na kuridhika kwa wateja.
Habari Picha 13352
Ametoa maelekezo kwa TTCL, kwa kulitaka   kuhakikisha Awamu ya Pili ya Mradi wa Faiba Mlangoni Kwako (Fiber to the Home – FTTH) na kwamba unufaisha wananchi kwa kuwapatia huduma yenye ubora, uhakika na gharama nafuu.
Ameielekeza TTCL kupanua wigo wa huduma ya faiba kwa kuhakikisha inafika katika maeneo yenye makazi yanayokua, masoko, maeneo ya biashara, viwanda, shule, vyuo, vituo vya afya na ofisi za Serikali Tanzania Bara na Zanzibar.
Vilevile kudumisha ubora wa huduma na kuimarisha huduma kwa wateja, ikiwemo kuhakikisha malalamiko yanashughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi.

Aidha ameielekea TTCL  kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa gharama nafuu kwa kuandaa vifurushi vinavyokidhi uwezo wa familia, wanafunzi, vijana na wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Habari Picha 13353
“Mradi wa Faiba Mlangoni Kwako si ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano pekee, bali ni hatua ya kimkakati ya kufungua fursa za elimu, biashara, ajira na ubunifu,  na kuchochea ujenzi wa uchumi wa kidijitali nchini,” amesema.

Amesisitiza uwajibikaji na nidhamu ya kibiashara katika usimamizi wa mradi, akitaka wazabuni na wakandarasi wasimamiwe kwa ufanisi ili kazi zikamilike kwa wakati, kwa ubora na kwa kuzingatia thamani ya fedha inayowekezwa.

Amesema mradi huo unaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidijitali 2024–2034, unaolenga kuongeza matumizi ya teknolojia na upatikanaji wa huduma za Serikali kwa njia ya kidijitali.

Waziri Kairuki, amesema katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050  ambayo inakusudia kuhakikisha ifikapo mwaka 2050 angalau asilimia 70 ya wananchi wanatumia TEHAMA, huku zaidi ya asilimia 80 ya huduma za Serikali zikipatikana kwa njia ya kidijitali iliyo salama na jumuishi.

Habari Picha 13354

Akitumia takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa robo mwaka iliyoishia Juni 2026, Waziri Kairuki amesema usajili wa intaneti nchini umefikia 62,793,986, huku matumizi ya data yakifikia Petabaiti 1,041.

Hata hivyo, amesema usajili wa huduma ya Faiba Nyumbani ulikuwa 178,904, hali inayoonyesha kuwa bado kuna fursa kubwa ya kukuza huduma ya intaneti ya kasi kupitia teknolojia ya nyuzi za macho.

Kwa upande  wake, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL,  Moremi Marwa, amesema awamu ya Pili ya Mradi wa Faiba Mlangoni Kwako ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Biashara wa Miaka 10 wa Shirika kwa kipindi cha 2025/26 hadi 2034/35, unaolenga kuimarisha na kuboresha huduma za mawasiliano nchini.

Amesema TTCL imeingia katika Awamu ya Pili ikiwa tayari imejenga msingi muhimu kupitia utekelezaji wa Awamu ya Kwanza, iliyolenga maeneo mbalimbali ya kimkakati nchini.

Amesema katika Awamu ya Kwanza, TTCL imefanikiwa kujenga zaidi ya Home Pass 280,000, huku jumla ya maungio ya huduma ya nyuzi za macho yakifikia karibu 300,000 nchini.

Habari Picha 13355
Amesema katika  Awamu ya Pili, amesema TTCL inalenga kuongeza zaidi ya Home Pass 400,000, hatua inayotarajiwa kupanua wigo wa upatikanaji wa intaneti ya kasi kwa wananchi, taasisi na wafanyabiashara.

Aidha amesema utekelezaji wa mradi huo unafanyika kwa ushirikiano na makandarasi wa ndani na wa kimataifa, wakiwemo Huawei, ZTT na Visoll, katika ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya nyuzi za macho.

Habari Picha 13356

Amesema ushirikiano huo ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha upanuzi wa mtandao unafanyika kwa kutumia teknolojia za kisasa na kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya huduma za intaneti nchini.

Mradi huo unalenga pia kuchochea matumizi ya teknolojia katika shughuli za kila siku, biashara, elimu na huduma za Serikali, sambamba na kuongeza fursa za kiuchumi kupitia upatikanaji wa intaneti yenye kasi na uhakika.

You Might Also Like

Watu Milioni 300 Afrika Kutumia Nishati Ya Umeme Ifikapi 2030-Biteko

TASU yaiomba serikali inunue kutoa ajira kwa mabaharia

TASAC yahadharisha wavuvi, wasafirishaji majini kuhusu upepo mkali

Taifa Gas Yaendelea Kuongoza Kampeni ya Nishati Safi kwa Taasisi na Sekta ya Utalii Tanzania

NIDA Yapata Kibali Maalum Kurekebisha Taarifa Kwa Walioghushi Ili  Kujisajili

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article BRELA Yatoa Elimu ya Hataza na Alama za Biashara kwa Wabunifu
Next Article Bunifu Ya Dawa Ya Mayai Kupunguza Hasara Kwa Wafugaji Wa Kuku
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bunifu Ya Dawa Ya Mayai Kupunguza Hasara Kwa Wafugaji Wa Kuku
Makala August 22, 2026
BRELA Yatoa Elimu ya Hataza na Alama za Biashara kwa Wabunifu
Habari August 21, 2026
ARU  Wabuni Utengenezaji Vigae Kutumia  Chupa Za Plastiki Za Vinywaji Vya Kuongeza Nguvu
Habari August 21, 2026
Kutoka Sh. Milioni 20 Hadi Uchumi Wa Bilioni : Ubunifu Wa Dkt. Cecilia China Unaunganisha Korosho, Mifugo, Viwanda Na Ajira
Makala August 21, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?