MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt. Nchemba: TPHPA Yazidi Kuwafikia Wakulima
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt. Nchemba: TPHPA Yazidi Kuwafikia Wakulima
Habari

Dkt. Nchemba: TPHPA Yazidi Kuwafikia Wakulima

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa mchango wake katika kuimarisha afya ya mimea na kuongeza tija ya kilimo, akisema juhudi hizo zinaendana na azma ya Serikali ya kuhakikisha usalama wa chakula na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo leo, Agosti mosi, mwaka huu 2026 alipotembelea banda la TPHPA wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya 33 ya Wakulima (Nanenane) 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
Habari Picha 12970
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru, ambaye amemweleza kuwa mamlaka hiyo imeongeza juhudi za kudhibiti visumbufu na magonjwa ya mimea, kutoa elimu kuhusu matumizi salama ya viuatilifu na kuimarisha huduma za afya ya mimea ili kuongeza uzalishaji na kipato cha wakulima.
Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Dkt. Nchemba amesema utendaji wa TPHPA unaakisi utekelezaji wa kaulimbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu 2026 isemayo, “Tambua Soko, Ongeza Tija, Tekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”
Ameitaka mamlaka hiyo kuendelea kuwafikia wakulima wengi zaidi kwa huduma za kitaalamu, ili kulinda mazao dhidi ya magonjwa na wadudu waharibifu, kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuimarisha usalama wa chakula nchini.
Habari Picha 12971
Habari Picha 12972
Habari Picha 12973
Habari Picha 12974
Habari Picha 12975
Habari Picha 12976

You Might Also Like

Utafiti Wa Nguvu Kazi, Mapato Ya Kaya Kutoa Taswira Mpya Ya Maendeleo

Pato la Mwananchi Lapanda Tabora

Kikwete: Waambieni Tunataka Maendeleo Sio Maneno

Profesa Kabudi Atoa Maagizo Mazito Bodi Ya Ithibati Ya Waandishi Wa Habari

Ridhiwani Aipongeza EWURA kwa Utoaji wa Huduma kwa Wananchi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article BRELA Kutumia Maonesho Ya Nanenane Kutoa Huduma Kuhusu Mfumo Ulioboreshwa
Next Article Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lawataka Wakulima Kutumia Nanenane Kujifunza Kilimo Cha Kisasa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania
Makala August 1, 2026
TVLA Yazalisha Chanjo ya Kudhibiti Homa ya Kutupa Mimba kwa Mifugo
Habari August 1, 2026
Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lawataka Wakulima Kutumia Nanenane Kujifunza Kilimo Cha Kisasa
Habari August 1, 2026
BRELA Kutumia Maonesho Ya Nanenane Kutoa Huduma Kuhusu Mfumo Ulioboreshwa
Habari August 1, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?