MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Makala

Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
5 Min Read
Na Lucy Ngowi
MWAKA 2022, ndani ya kundi la vijana wabunifu waliokusanyika kuwasilisha mawazo yao kwenye shindano la ubunifu lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kulikuwa na wazo moja lililolenga kutatua changamoto ambayo wakulima wengi wa Tanzania wameiishi kwa miaka mingi ambayo ni kupanda mbegu kwa gharama kubwa, nguvu nyingi na tija ndogo.
Leo, miaka minne baadaye, wazo hilo limegeuka kuwa Rafiki Planter, teknolojia rahisi ya kupandia mbegu inayobadilisha namna kilimo kinavyofanyika.
Kwa wabunifu wake, safari hiyo ni ushahidi kuwa miaka 40 ya COSTECH imekuwa safari ya kuibua vipaji, kulea ubunifu na kugeuza mawazo ya Watanzania kuwa suluhisho la maendeleo ya Taifa.
Ubunifu huo ulifanywa na watafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Kituo cha Ukiriguru, Mwanza, wakiongozwa na Dawson Malela, kwa kushirikiana na Dkt. Paul Saidia na Robert Cheleo.
Malela anasema awali walitengeneza mashine ndogo iliyokuwa na injini ya CC 125 na magurudumu ya chuma ili kuhimili mazingira ya shambani, ikiaminika kwamba matumizi ya matairi ya mpira yangeweza kupata pancha.
Habari Picha 12896
Walidhani wamepata suluhisho, lakini walipoipeleka kwa wakulima wakagundua ubunifu hauishii katika karakana bali huendelea shambani kupitia maoni ya watumiaji.
“Wakulima walituambia wanahitaji mashine yenye injini yenye uwezo mkubwa zaidi na inayoweza kufanya kazi muda mrefu bila kupata joto. Pia walihitaji mashine iwe na magurudumu makubwa zaidi yanayofaa kwenye mazingira mbalimbali ya mashamba. Tulipokea maoni yao na kuanza maboresho,” anasema.
Lakini maboresho hayo yasingewezekana bila taasisi iliyokuwa tayari kuamini ndoto yao.
“COSTECH ndiyo waliotushika mkono mwanzoni kabisa kupitia mashindano ya kitaifa ya Sayansi teknolojia na ubunifu maarufu kama MAKISATU. Tulipoibuka washindi wa shindano la ubunifu mwaka 2022, walitupatia rasilimali za kuwezesha utengenezaji wa  mashine imara, walituunganisha na wahandisi waliokuwa wakifanya kazi nasi bega kwa bega na walitusaidia hadi katika hatua za usajili na ulinzi wa teknolojia yetu. Hapo ndipo safari ya mafanikio ya Rafiki Planter ilipoanza,” anasisitiza Malela.
Anasema COSTECH haikutoa fedha pekee, bali ilitoa mazingira ya ubunifu kukua. Wataalamu wake waliendelea kuwapa ushauri kila walipokutana na changamoto, hatua iliyowajengea uwezo wa kuboresha teknolojia yao kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wakulima.
Baadaye, Wizara ya Kilimo kupitia Mradi wa Tanzania Food Systems Resilience Program (TFSRP) iliendelea kuunga mkono maboresho hayo, na kufanya Rafiki Planter kuwa teknolojia yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuongeza tija ya uzalishaji.
Leo, mashine hiyo imekuwa na ufanisi mkubwa, kwani inaweza kupanda ekari moja ndani ya dakika 45 hadi saa moja, kazi ambayo kwa kutumia jembe la mkono inaweza kuchukua zaidi ya saa nane na kuhitaji watu wengi.
 Zaidi ya hayo, mashine hupanda mbegu kwa nafasi sahihi zinazopendekezwa kitaalamu, jambo linaloongeza idadi ya mimea na mavuno.
Kwa mfano, katika zao la alizeti, mkulima anayepanda kwa kutumia nafasi sahihi anaweza kuvuna magunia 12 hadi 15 kwa ekari badala ya magunia matano au sita yanayopatikana mara nyingi kwa upandaji usiozingatia viwango.
Faida nyingine ni kwamba Rafiki Planter inaweza kuendeshwa na mwanaume au mwanamke, hivyo kuwafanya wanawake na vijana kushiriki kwa urahisi katika kilimo chenye tija.
Hii inaendana na azma ya Serikali ya kuwavutia vijana kwenye sekta ya kilimo kwa kutumia teknolojia zinazorahisisha kazi.
Kwa Malela, mafanikio ya Rafiki Planter ni ushahidi kuwa uwekezaji wa Serikali katika sayansi, teknolojia na ubunifu una matokeo yanayoonekana. Anaamini kuwa kupitia COSTECH, mamia ya wabunifu wa Kitanzania wamepata nafasi ya kubadilisha mawazo yao kuwa bidhaa na teknolojia zinazoweza kutatua changamoto za wananchi.
Kadiri COSTECH inavyoadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake, hadithi ya Rafiki Planter inaonyesha kuwa maendeleo ya Taifa hayawezi kutenganishwa na uwekezaji katika sayansi, teknoloojia na ubunifu.
Ofisa mwandamizi wa COSTECH katika Mfuko wa Taifa wa uendelezaji Sayansi na teknolojia (MTUSATE), Ntufye Mwakigonja, anaelezea kuwa uwezeshaji uliofanyika kwenye ubunifu wa Rafiki planter, ni sehemu ya majukumu mapana ya Tume katika kusukuma gurudumu la teknolojia nchini.
Anasema tangu kufungua dirisha la ubunifu katika mfuko wa MTUSATE, Tume imekwisha tambua wabunifu zaidi ya 3000 kote nchini.
Aidha, takribani wabunifu 350 wamewezeshwa kwa kupatiwa mafunzo, fedha na kuunganishwa na taasisi mbalimbali zinazochangia uundaji wa teknolojia husika.
Akimwelezea Malela, Mwakigonja anasema COSTECH ilitoa fedha za kitanzania ili kugharamia maboresho ya teknolojia ya rafiki planter.
Katika hatua ya awali, mbunifu alikuja na sampuli kifani ambayo ilikuwa na uwezo mdogo. Hivyo kiasi cha fedha kilichotolewa kiliwezesha kufikisha teknolojia hiyo katika hatua iliyopo sasa.

You Might Also Like

Kenya, Tanzania Zashirikiana na China Kukabiliana na Changamoto za Ushuru wa Marekani

Daraja La Magufuli Laimarisha Uhusiano Wa Jumuiya Ya China,Tanzania Yenye Mustakabali Wa Pamoja

MATUKIO YA MISIBA KWA WATU MAARUFU YALIYOJIRI KUANZIA JANUARI 2024, HADI DISEMBA 2024

Madaktari Toka China Waleta Matumaini Barani Afrika

Sanaa, Utamaduni Yaimarisha Urafiki Wa China, Afrika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Watendaji Wakuu Waagizwa Kuifanya Dira 2050 Kuwa Mwongozo Wa Maamuzi Yao
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Watendaji Wakuu Waagizwa Kuifanya Dira 2050 Kuwa Mwongozo Wa Maamuzi Yao
Habari July 24, 2026
Nchi za SADC Zahimizwa Kuimarisha Umoja Kukabili Changamoto
Uncategorized July 17, 2026
Wananchi Washauriwa Kutumia  Wataalam Wa Ujenzi Kuepuka Madhara
Habari July 14, 2026
July 14, 2026
Uncategorized July 14, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?