MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Katambi Apongeza Zimamoto Kwa Uwekezaji Wa Vifaa Vya Kisasa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Katambi Apongeza Zimamoto Kwa Uwekezaji Wa Vifaa Vya Kisasa
Uncategorized

Katambi Apongeza Zimamoto Kwa Uwekezaji Wa Vifaa Vya Kisasa

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Lyatuu
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Paschal Katambi Patrobass, ametembelea Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo,  Katambi amepata fursa ya kutembelea na kujionea vifaa na mitambo mbalimbali ya kisasa inayotumiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika shughuli za kuzima moto, uokoaji na kukabiliana na majanga mbalimbali.
Habari Picha 12725
 Vifaa hivyo ni sehemu ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa lengo la kuimarisha uwezo wa Jeshi katika kulinda maisha na mali za wananchi.
Maofisa wa Jeshi walimpa Waziri maelezo kuhusu matumizi ya vifaa hivyo, uwezo wake wa kukabiliana na matukio mbalimbali ya dharura, pamoja na namna vinavyorahisisha utoaji wa huduma za haraka na zenye ufanisi kwa wananchi.
Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Katambi amelipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuendelea kuimarisha uwezo wake wa kitaalamu na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Habari Picha 12726
Aidha, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu  kuendelea kuwekeza katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vinavyoongeza uwezo wa Jeshi kukabiliana na majanga na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kwa upande wake, uongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji umemshukuru Waziri kwa kutembelea banda hilo na kuendelea kutoa ushirikiano na mwelekeo unaowezesha Jeshi kuendelea kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kutumia Maonesho ya Sabasaba kutoa elimu kwa umma kuhusu kinga dhidi ya majanga ya moto, tahadhari za usalama, huduma za uokoaji, pamoja na kuhamasisha wananchi kupiga namba ya dharura 114 wanapokumbana na matukio ya moto au dharura nyingine zinazohitaji huduma za Jeshi.
Habari Picha 12725

You Might Also Like

Vinasaba 524 Vimepimwa Kwa Mkemia Mkuu

Dkt Biteko Ahimiza Watanzania Kupiga Kura Novemba 27,2024

Waziri Jenista akabidhiwa ofisi rasmi na Ummy Mwalimu

Profesa Kabudi Amimina Pongezi TEA

Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi,waweke pingamizi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Habari June 29, 2026
Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi
Habari June 29, 2026
WCF Yapigia Debe Ushirikiano na Teknolojia Kuimarisha Hifadhi ya Jamii
Habari June 28, 2026
Sabasaba 2026 Kuingiza Teknolojia Mpya na Fursa za Uwekezaji
Habari June 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?