MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wadau wataka mifumo jumuishi kupunguza mzigo wa malezi kwa wenye ulemavu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wadau wataka mifumo jumuishi kupunguza mzigo wa malezi kwa wenye ulemavu
Habari

Wadau wataka mifumo jumuishi kupunguza mzigo wa malezi kwa wenye ulemavu

Author
By Author
Share
5 Min Read

Na Lucy Lyatuu

WADAU wa haki za watu wenye ulemavu wameitaka serikali na taasisi mbalimbali nchini kuimarisha mifumo jumuishi ya huduma za kijamii, kiuchumi na sera ili kupunguza mzigo wa kazi za malezi kwa watu wenye ulemavu, wakisema changamoto hiyo inaendelea kuwaathiri zaidi wanawake, vijana na wasichana wanaobeba jukumu kubwa la kutoa huduma bila malipo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Susan Ngongi Namondo wakati wa Mjadala wa Kitaifa wa Kuchunguza Mwingiliano kati ya Kazi za Ulezi Zisizolipwa na Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania.

Habari Picha 12181

Amesema kuna umuhimu wa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa kikamilifu katika kufanya maamuzi ili sera na mipango mbalimbali iweze kuandaliwa kwa kushirikiana nao.

“Ujumuishaji wa watu wenye ulemavu haupaswi kuishia kwenye miundombinu au teknolojia pekee, bali pia ujengwe kupitia ushirikiano wa kijamii, fursa za kiuchumi na mifumo ya maendeleo inayowawezesha kuchangia katika ustawi wa taifa,”amesema.

Habari Picha 12182

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Watu Wenye Ulemavu, Dk Ali Omar amesema bado kuna changamoto kubwa zinazowakabili watu wenye ulemavu katika kupata huduma za kila siku, elimu, afya pamoja na kujitafutia kipato kutokana na kazi za ulezi zisizolipwa.

Amesema hali hiyo inaathiri ustawi wa wanawake, vijana na wasichana wenye ulemavu katika jamii.

Omar amesema ripoti iliyowasilishwa katika mjadala huo itasaidia kutoa mwongozo wa kuboresha huduma na kuongeza uelewa kuhusu mahitaji ya watu wenye ulemavu huku akiwashukuru wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuendelea kuimarisha ustawi na haki za kundi hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa haki za watu wenye ulemavu, Neema Kalole amesema utafiti huo umefungua uelewa mpya kuhusu changamoto zinazowakabili watu wanaotoa huduma za malezi kwa watu wenye ulemavu.

Habari Picha 12183

Amesema mara nyingi mjadala hujikita kwa mtu mwenye ulemavu pekee huku walezi na watoa huduma wakisahaulika licha ya kuwa na mchango mkubwa katika maisha ya kila siku ya watu wenye ulemavu.

“Mara nyingi tunamsikiliza zaidi mtu mwenye ulemavu lakini mara chache sana tunamsikiliza anayemsaidia. Utafiti huu umetufundisha namna ya kuboresha utetezi wa haki za watu wenye ulemavu pamoja na kuwajumuisha walezi katika sera na mipango ya maendeleo,” amesema Kalole.

Mratibu wa Mradi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ghati Horombe amesema mradi huo unatekelezwa Tanzania kwa ushirikiano wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo UNDP, UN Women na UNFPA chini ya ufadhili wa Global Disability Fund.

Amesema mradi huo unalenga kujenga uelewa mpana kwa watunga sera, taasisi za serikali na mashirika ya watu wenye ulemavu kuhusu changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu na wale wanaowahudumia.

Habari Picha 12184

Horombe amesema tafiti zilizofanyika zimebaini changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma katika maeneo ya vijijini wakati watu wengi wenye ulemavu wanaishi huko.

“Tumebaini kuwa huduma nyingi muhimu ziko mijini wakati watu wengi wenye ulemavu wanaishi vijijini, jambo ambalo linaongeza ugumu wa kupata huduma za afya, elimu na vifaa saidizi,” amesema.

Kwa upande wake Mchambuzi wa Idadi ya Watu na Maendeleo wa UNFPA, Ramadhan Hangua amesema takwimu zinaonesha ongezeko la uelewa kuhusu watu wenye ulemavu nchini.

Amesma Sensa ya mwaka 2002 ilionesha watu wawili kati ya 100 wana aina moja au zaidi ya ulemavu, mwaka 2012 idadi hiyo iliongezeka hadi watu tisa kati ya 100 huku sensa ya mwaka 2022 ikionesha watu 11 kati ya 100 wanaishi na aina moja au zaidi ya ulemavu.

Hangua amesema ongezeko hilo halimaanishi kuongezeka kwa watu wenye ulemavu pekee, bali pia kuongezeka kwa uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kuwatambua na kuwahesabu watu wenye ulemavu.

Habari Picha 12185

Naye Mtafiti Msaidizi wa UN Women, Perpetua Senkoro amesema utafiti huo umebaini changamoto kubwa katika mifumo ya usafiri, miundombinu na upatikanaji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu.

Amesema ukosefu wa vifaa saidizi vinavyokidhi mahitaji husababisha watu wenye ulemavu kushindwa kujitegemea na kuongeza mzigo kwa walezi na watoa huduma.

Aidha amesema changamoto ya kiuchumi imeonekana kuwa kikwazo kikubwa kwa watu wenye ulemavu na walezi wao, huku akipendekeza kuwepo kwa maboresho ya sera, bajeti na mifumo ya mikopo ili kuwafikia pia watu wanaowahudumia watu wenye ulemavu.

 

You Might Also Like

Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara

Umeme Vitongojini Wachoche Uchakataji Mazao Katavi

Mkenda: Maendeleo ya Taifa Yanategemea Sayansi na Teknolojia

Serikali Yazindua Soko Kuu Jipya la Kariakoo Baada ya Moto wa 2021

Wataalamu wa Fedha SADC Wakutana Pretoria Kujadili Bajeti

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wabunge Waitaka Ujenzi Kuwa Na Mageuzi Makubwa Ya Ujenzi Wa Barabara
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wabunge Waitaka Ujenzi Kuwa Na Mageuzi Makubwa Ya Ujenzi Wa Barabara
Habari May 21, 2026
Wizara Ya  Ujenzi Kutekeleza Vipaumbele Sita,Ujenzi Wa Miundombinu
Habari May 20, 2026
Wizara ya Maji: Uhifadhi Ziwa Victoria Unahitaji Ushirikiano, Uwekezaji Endelevu
Habari May 20, 2026
MAIPAC NA THRDC Watoa Mafunzo Kwa Waandishi Wa Habari Za Mazingira, Kanda Ya Ziwa
Habari May 20, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?