MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Sh. Bilioni 883.93 Zatumika Kutekeleza Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Sh. Bilioni 883.93 Zatumika Kutekeleza Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira
Habari

Sh. Bilioni 883.93 Zatumika Kutekeleza Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, amesema Sh. Bilioni 883.93, sawa na Dola za Marekani milioni 351.04, zimetumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maji na usafi wa mazingira nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mapitio ya Pamoja wa Sekta ya Maji, ulioandaliwa na Wizara ya Maji mjini Morogoro, Balozi Khamis amesema fedha hizo zilipatikana kutoka kwa wadau wa maendeleo na vyanzo vya ndani vya serikali.
Mkutano huo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Siku ya Maji Duniani, itakayoadhimishwa Machi 22, mwaka huu 2026.
Habari Picha 11516
Balozi Khamis pia ameipongeza Sekta ya Maji kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa miaka 20 ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP).
Amesema tangu kuzinduliwa mwaka 2006, huduma ya maji mjini imeongezeka kutoka asilimia 74 hadi 92.5, na vijijini kutoka asilimia 54 hadi 85.2.
Aidha, alibainisha kuwa mkutano huo ni jukwaa la ngazi ya juu la majadiliano na tathmini ya utekelezaji wa WSDP, huku akisisitiza umuhimu wa wadau kushirikiana katika kuhakikisha upatikanaji wa maji unaendelea kuboreshwa.
Habari Picha 11517
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa maji nchini unafikia asilimia 100.
“Hadi sasa, vijiji 10,758 tayari vimeshapata huduma ya maji ya uhakika, huku vijiji 1,575 bado vikiwa nyuma,” amesema.
Amesisitiza kuwa miradi mikubwa ikiwemo Mpango wa Gridi ya Taifa ya Maji inaendelea kutekelezwa ili kufikia malengo hayo.
Mwajuma ameongeza kuwa mkutano huo ni fursa ya wadau kushirikiana, kuchambua mafanikio na changamoto zilizojitokeza, na kupanga mikakati ya utekelezaji wa WSDP awamu ya tatu kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2025.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kigoma Malima, amemshukuru Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, na watendaji wa wizara kwa kufanya maadhimisho ya Wiki ya Maji Mkoani Morogoro.
Amesema mkoa wa Morogoro ni mdau muhimu wa sekta ya maji na unatambua jukumu lake la kuhifadhi vyanzo vya maji, kwani ni chanzo kikuu cha maji kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

You Might Also Like

Mjadala na Kampuni za Nishati Kimataifa Kuendelezwa

PIC Uwekezaji Bidhaa Za Ngozi Utaongeza Mapato

Vyombo vya Habari ni Kama Maji’ -Biteko 

Tanzania Kushirikiana na Finland Uboreshaji Mbegu za Miti

Sierra Leone Yaipongeza TARURAUjenzi Wa Madaraja, Barabara Za Mawe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Jamii Yatakiwa Kuzungumza Pamoja Kuhusu Maji, Masuala ya Jinsia
Next Article Uwekezaji wa NSSF wa Mzizima Towers Kufungua Fursa Mpya za Biashara na Utalii Dar
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

VETA  Yapongezwa Kwa Kuibua Vipaji Kwa Vijana  
Habari June 24, 2026
Kundi Kubwa La Wanafunzi Hukatisha Masomo Katika Ngazi Mbalimbali Ya Elimu -TEWW 
Habari June 24, 2026
TEMESA  Yajadhimisha Miaka 20, Yajivunia  Mafanikio  Na Kuahidi  Kuimarisha  Huduma
Habari June 24, 2026
PURA Yasema Tanzania Inaendelea Kujivunia Uwepo Wa Gesi Asilia,Ni Nguzo Muhimu Katika Kuchochea Maendeleo
Habari June 24, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?