MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Pinda Aitaka Jamii Kujikita Upandaji Miti Bila Kusubiri Matukio Maalumu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Pinda Aitaka Jamii Kujikita Upandaji Miti Bila Kusubiri Matukio Maalumu
Habari

Pinda Aitaka Jamii Kujikita Upandaji Miti Bila Kusubiri Matukio Maalumu

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
4 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, ameitaka jamii kuacha kusubiri matukio maalumu ya viongozi ili kuanza kupanda miti, na badala yake kufanya zoezi hilo kuwa endelevu kama sehemu ya maisha ya kila siku, hatua itakayosaidia juhudi za Serikali katika kutunza na kulinda mazingira nchini.
Pinda ameyasema hayo leo Februari 6, 2026  jijini Dodoma wakati wa zoezi la upandaji miti 1,000 lililofanyika katika eneo la Njedengwa, mkoani Dodoma.
Zoezi hilo lilihusisha Taasisi ya Habari Conservation, wakazi wa eneo hilo pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali.
Amesema jamii haipaswi kusubiri matukio maalumu, kama vile siku za kuzaliwa za viongozi, ili kuanzisha kampeni za upandaji miti, bali ihakikishe kuwa kupanda na kutunza miti kunakuwa tabia endelevu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
“Wananchi kuanzia ngazi ya kata hadi taifa kwa ujumla tunapaswa kuwa na utaratibu wa kupanda miti bila kusubiri msukumo kutoka kwa viongozi.
“Mfano, siku ya kuzaliwa ya Rais isiwe kigezo pekee, bali tujitoe wenyewe kila wakati,” amesema Pinda.
Ameongeza kuwa lengo ni kuona kila Mtanzania anatambua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti ya aina mbalimbali, ikiwemo ya kivuli na ya matunda, ili kuchangia kuboresha hali ya hewa na ustawi wa maisha ya jamii.
Aidha, amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Taasisi ya Habari Conservation kutumia vikundi vya vijana, hususan wale wanaofanya mazoezi ya asubuhi kama kukimbia, kuwahamasisha kushiriki katika kampeni za upandaji miti katika maeneo mbalimbali.
Pinda amesema vijana wana nguvu na ushawishi mkubwa katika jamii, hivyo wakitumika ipasavyo wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika suala la uhifadhi wa mazingira.
Habari Picha 11121
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kudhibiti Manunuzi ya Umma (PPRA), Dennis Simba, ameipongeza Taasisi ya Habari Conservation kwa kujikita katika masuala ya mazingira kwa lengo la kuisaidia Serikali kuboresha na kutunza mazingira.
Simba amesema PPRA imeingia makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja na taasisi hiyo baada ya kujiunga na mfumo wa NesT unaotumiwa na Serikali katika manunuzi.
Ameongeza kuwa ushirikiano huo utawezesha kuhakikisha miti iliyopandwa katika eneo la Njedengwa na maeneo mengine inatunzwa ipasavyo.
Amesema kwa sasa PPRA imekuwa mdau mkubwa wa mazingira, na akaziomba taasisi nyingine kujiunga na mfumo wa NesT ili kwenda kidigitali, kuboresha uwazi katika manunuzi na kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo uhifadhi wa mazingira.
Habari Picha 11122
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema mkakati wa mkoa ni kuhakikisha maeneo yote yaliyoainishwa yanapandwa miti kwa lengo la kutunza mazingira na kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema katika msimu uliopita mkoa ulifanikiwa kupanda miti 40,000, huku matarajio yakiwa ni kuongeza idadi hiyo katika misimu ijayo ili kufikia malengo ya mkoa katika uhifadhi wa mazingira.
Naye mwakilishi wa Taasisi ya Habari Conservation, Loyce Obongo, amesema taasisi hiyo imejipanga kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine katika kutekeleza miradi ya upandaji na utunzaji wa miti, kwa lengo la kuboresha mazingira na kuhamasisha jamii kuchukua wajibu wao.

You Might Also Like

Ridhiwani, Ulega Washiriki Maulid Ya Kumswalia Mtume Muhammad

Katambi Aagiza Ushindani Wa Haki Ili Kulinda Bei, Walaji

Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi

Serikali Yatumia Zaidi Ya Bilioni 100 Kupeleka Umeme Simiyu

TPHPA Tumejiimarisha Kudhibiti Visumbufu Vya Mazao – Ndunguru

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tanzania Yaongeza Kasi ya Utafutaji Masoko ya Parachichi Ulaya
Next Article Dkt. Ikomba Wa CWT Asema, Walimu Wanafanya Kazi Zaidi Bila Kulipwa Stahiki Zao
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Kisasa Design: Kampuni ya Kitanzania Inayobadilisha Sekta ya Interior Design na Utengenezaji wa Samani
Habari June 6, 2026
Vidukari Hatari Vyafuatiliwa Mikoa 17 Kulinda Zao la Mpunga
Makala June 5, 2026
KARIBU ESCAPE LODGE SERENGETI – NYUMBA YAKO YA KIFAHARI KATIKATI YA UFALME WA WANYAMAPORI
Habari June 5, 2026
Sheria Ya  Kuzuia Shisha Kutungwa, Yabainika Kuwekwa Dawa Za Kulevya
Habari May 29, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?