MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Umeme Vitongojini Wachoche Uchakataji Mazao Katavi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Umeme Vitongojini Wachoche Uchakataji Mazao Katavi
Habari

Umeme Vitongojini Wachoche Uchakataji Mazao Katavi

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
IMEELEZWA  kuwa mradi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Awamu ya Pili B (HEP 2B) unatarajia  kuongeza  na kuchocchea uchakataji wa mazao ambayo kwa kiasi kikubwa wananchi wa mkoa wa Katavi wanazalisha mazao katika mkoa huo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,  Mwanamvua Mrindoto leo  Februari 6,2026 mara baada ya kutambulishwa kwake mkandarasi Kampuni ya M/s ETDCO Ltd atakayetekeleza mradi wa HEP 2B wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 358 kwa wakazi zaidi ya 11,536 mkoani Katavi.
“Kwa sasa  badala ya kuuza mazao ghafi tutaiza bidhaa, suala hili la kupatikana kwa umeme litakwenda kuipandisha bei za mazao kwa sababu yatachakatwa katika hali nzuri na zitauzwa bidhaa badala ya kuuza malighafi,” Amesema Mrindoto.
Vilevile, ameongeza kuwa upatikanaji wa umeme wa uhakika kupitia mradi wa HEP 2B utakwenda kukuza uchumi, kukuza uwekezaji na kuleta ajira kwa vijana, wanawake, wazee na makundi mbalimbali katika mkoa huo.
“Nimsisitize mkandarasi kujipanga sawasawa uingie kazini kwa miguu yote miwili ukiwa na kasi kubwa kwa sababu wanachohitaji wananchi ni umeme wala sio maneno au ahadi, sio ratiba, sio michakato,” Amesema Mrindoto.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA,  Mussa Muze amesema lengo kuu la utekelezaji wa mradi wa HEP 2B ni kuongeza upatikanaji wa umeme kwa wananchi katika vitongoji vya mkoa wa Katavi na kusaidia maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi.
Naye, Msimamizi wa Miradi ya REA mkoa wa Katavi, Gilbert Furia amesema, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Katavi kushiriki vema katika utekelezaji wa mradi, na kutumia fursa ya kuletewa umeme  kuweza kujiinua kiuchumi.
Pia, Mkandarasi kutoka Kampuni ya M/s ETDCO Ltd, Abdalah Mitenda amemueleza Mrindoto kuwa katika mradi huo wakandarasi watapewa kipaumbele kufanya shughuli mbalimbali zitakazokuwa zinafanyika katika mradi huo na kuwataka kuchangamkia fursa.

You Might Also Like

Brela Yatoa Huduma Zote Za Usajili Katika Maonesho Ya Teknolojia Ya Madini Geita

Tanzania Yatumia Wiki Ya Nishari India Kunadi Vitalu Vya Mafuta Na Gesi Asilia

Mwalim: Niko Tayari Kushirikiana na Majaliwa Nikipewa Ridhaa ya Urais

TUGHE Yatoa Wito Kwa Wafanyakazi Kujitokeza Kupiga Kura

Mwalim: Ardhi Yetu ni Ufunguo wa Uhuru wa Kiuchumi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Taska Mbogo Aitaka Serikali Kurejesha Viwanda, Kuimarisha Kilimo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Taska Mbogo Aitaka Serikali Kurejesha Viwanda, Kuimarisha Kilimo
Habari February 6, 2026
Makampuni 408 Ya Tanzania Yaruhusiwa Kusafirisha Mazao Ya Kilimo Kwenda China
Habari February 5, 2026
Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara
Habari February 5, 2026
TEHAMA Kuchochea Uchumi wa Kidijitali, Serikali Yatenga Sh Bil Tano Kwa Kampuni Changa
Habari February 5, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?