MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala

Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Ilongelo, Hidary Gulamali, ameibua hoja Bungeni akiitaka Serikali kueleza mpango wake wa kuboresha huduma za mawasiliano kwa kujenga minara ya simu katika maeneo yenye changamoto ya mtandao na mawasiliano ya simu ndani ya jimbo lake.
Gulamali ametoa hoja hiyo wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Bunge kilichofanyika jijini Dodoma, akieleza kuwa ukosefu wa mawasiliano ya uhakika umekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi, hasa katika nyanja za kiuchumi, elimu na shughuli za kijamii.
Amezitaja kata za Namuhunga na Ilongelo kuwa miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi, ambapo wananchi hulazimika kutembea umbali mrefu ili kupata huduma za simu na intaneti.
“Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga minara ya mawasiliano katika kata za Namuhunga na Ilongelo zilizopo Jimbo la Singida Vijijini?” alihoji mbunge huyo.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Switbert Mkama, amesema Serikali imeshatambua changamoto ya mawasiliano inayokabili maeneo mbalimbali nchini, hususan vijijini, na tayari imeanza kuchukua hatua za makusudi kuikabili.
Amefafanua kuwa Serikali imeandaa mkakati wa miaka mitano unaolenga kujenga minara ya mawasiliano katika maeneo yote yenye upungufu wa huduma hiyo, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano ya uhakika na yenye ubora.
Dkt. Mkama amemhakikishia mbunge huyo kuwa kata za Namuhunga na Ilongelo pamoja na maeneo mengine yenye changamoto katika Jimbo la Singida Vijijini zitahudumiwa kupitia utekelezaji wa mkakati huo pindi utakapotekelezwa kikamilifu.

You Might Also Like

Kiswahili Chavuka Mipaka, Paris Yajiandaa Kukipokea

Madaktari Toka China Waleta Matumaini Barani Afrika

Kinywaji Cha China Chavuka Mipaka Chatua Tanzania

Polisi Dar yashikilia watatu kwa mauaji ya mfanyakazi wa Kampuni ya Hope Recycling

Abubakar Assenga Aomba Ridhaa Ya Wananchi Wa Kilombero Wamchague Tena

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Next Article Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ziwa Ngozi Lavuta Mamia Sabasaba, Wageni Washangazwa Na Ramani Ya Afrika Juu Ya Mlima
Habari July 9, 2026
Shirika La Uzalishaji Mali La Polisi Kujenga Vituo Vya Ukaguzi Wa Vyombo Vya Moto
Habari July 9, 2026
Watumishi 7881 Watakaostaafu 2026/27 Watambuliwa Kupitia Kampeni Ya Tunalipa Jana-PSSF
Uncategorized July 8, 2026
Katambi Apongeza Zimamoto Kwa Uwekezaji Wa Vifaa Vya Kisasa
Uncategorized July 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?