MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPDC na PURA Hakikisheni Watanzania Wananufaika na Rasilimali za Mafuta na Gesi- Salome
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPDC na PURA Hakikisheni Watanzania Wananufaika na Rasilimali za Mafuta na Gesi- Salome
Habari

TPDC na PURA Hakikisheni Watanzania Wananufaika na Rasilimali za Mafuta na Gesi- Salome

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

NAIBU  Waziri wa Nishati  Salome Makamba amefanya ziara katika  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa lengo la kuzungumza na Watendaji taasisi hizo mara baada ya kuteuliwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika nyadhifa hiyo  ambapo amewataka watendaji kuhakikisha  Watanzania wananufaika moja kwa moja na uwepo wa rasilimali za mafuta na gesi.

Habari Picha 10529

 

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam,  Salome ameweka mkazo kuhusu upatikanaji wa ajira kwa Watanzania, huduma za kijamii na upatikanaji wa nishati kwa gharama nafuu.

 

Salome pia ameielekeza Menejimenti ya TPDC kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi asilia majumbani ili Watanzania waendelee kunufaika zaidi na rasilimali hiyo muhimu.

Habari Picha 10530

 

Vilevile  ameipongeza TPDC kwa jitihada wanazoendelea kufanya katika utafutaji na uendelezaji wa rasilimali za mafuta na gesi asilia nchini kwani uboreshaji huo umeanza kuleta matokeo chanya katika upatikanaji wa nishati hiyo katika maeneo mbalimbali nchini huku akiwataka kuhakikisha jitihada hizo zinawanufaisha wananchi wengi zaidi.

 

Katika hatua nyingine, . Salome amewapongeza PURA kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kuhakikisha sekta ya mafuta inakua nchini huku akiwahimiza kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanakuwa rafiki kwa wawekezaji wapya ili kuongeza ajira na kuhakikisha wananchi wanapata manufaa ya moja kwa moja kutokana na rasilimali na uwekezaji uliopo nchini.

 

Aidha, amesisitiza kuwa miradi ya utafiti na uendelezaji wa gesi asilia, ikiwemo mradi wa LNG, ipewe kipaumbele ili kuongeza tija katika uwekezaji na kuhakikisha nchi inanufaika kikamilifu na rasilimali zake huku akisisitiza kuwa taasisi zote zilizo chini ya Wizara lazima ziweke mbele maslahi ya wananchi wakati wa kusimamia miradi ya kimkakati ya nishati lakini pia kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu usimamizi, matumizi na faida za rasilimali za gesi asilia.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amewasisitiza TPDC kuongeza kasi ya uzalishaji na upatikanaji wa  gesi ili nishati hiyo iwe ya kutosha na inawafikia wananchi huku akiisisitiza PURA kuhakikisha wanawapa wawekezaji kipaumbele katika kuwekeza katika fursa za mafuta na gesi kwa lengo la kuhakikisha Serikali inapata mapato na wananchi wananufaika na miradi hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mussa Makame amesema shirika linaendelea kuimarisha miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha nishati ya mafuta na gesi, huku likiandaa vizuri upande wa maboresho ya masoko ili kuongeza ufanisi na upatikanaji wa bidhaa hizo nchini na kueleza kuwa kampuni ipo kwenye hatua za kufanya upanuzi wa miradi ya gesi, ikiwemo utekelezaji wa miradi midogo ya LNG itakayowezesha kusafirisha gesi hiyo katika mikoa mbalimbali kwa gharama nafuu na kwa wakati.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa PURA,  Charles Sangweni amesema PURA itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi huku ikichangia kufanikisha malengo ya sekta kwa mujibu wa Dira ya Taifa 2050.

 

You Might Also Like

Nchi Za SADC Zahimizwa Kutunza, Kulinda Amani

MSD, SALAMA Zaunganisha Nguvu Kuboresha Sekta ya Afya SADC

NHIF Kuingia Makubaliano Na Mawakala Usajili Wa Wananchi

Ajali Yakatisha Maisha Ya Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji TANESCO, Dereva Wake 

Daktari: Saratani ya Matiti Inazuilika, Inatibika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Kuanzisha Kituo Maalum Cha Kuwezesha Wawekezaji Vijana
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Kuanzisha Kituo Maalum Cha Kuwezesha Wawekezaji Vijana
Habari December 8, 2025
Mita  Janja Zazinduliwa,  Tanesco  Yatakiwa Kuzisambaza Nchi Nzima
Habari December 5, 2025
DIT Andaeni Taarifa  Itakayowezesha Wanafunzi Kupelekwa Nje Kujifunza-Mkenda
Habari December 5, 2025
Msama Aipongeza Hotuba Ya Samia, Atoa Neno Kwa Vijana, Wazee, Wanaharakati
Habari December 4, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?