Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 4

Mpango Wa Taifa Wa Teknolojia Uko Mbioni Kuja-Serikali

Na Lucy Lyatuu

SERIKALI imesema iko mbioni kutengeneza mpango wa taifa wa teknolojia ambao utapambanua mahitaji ya teknolojia  yalivyo ili kwamba vijana waweze kuleta bunifu zenye kujibu mahitaji ya jamii.

Kaimu Katibu Mkuu, kutoka Wizara ya Elimu Sayansi Na Teknolojia, Ladislaus Mnyone amesema hayo wakati akitoa zawadi na vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

Habari Picha 10493

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Carolyne Nombo, amesema mpango huo katika miaka 10-3 ijayo  utaongeza fursa  na kusaidia wabunifu kulitoa taifa kutoka  hatua moja hadi nyingine  hususani kwenye eneo la ubunifu.

Amesema nchi  ya Tanzania ina vituo vya umahiri 12 na kuwataka wabunifu kutoka DIT kuvitumi katika kushiriki kwenye masuala mbalimbali ili waweze kulelewa.

Amewataka vijana kutumia vizuri fursa  ya vituo vya umahiri vilivyopo  nchini ili kuleta chachu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini.

Habari Picha 10494

Kuhusu Taasisi hiyo kuwatambua wale waliofanya vizuri amesema ni  moja ya eneo linawezesha kuzalishwa kwa wingi teknolojia ambao zitatatua mahitaji yaliyopo katika jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo, Profesa  Preksedis Ndomba amesema chuo hicho hutoa zaidi za aina mbili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo  yao ambayo hutoa chachu kwao ili kuongeza bidii.

Amewataka wanafunzi hao ambao wanamaliza masomo yao kuwa kadri watakavyokuwa wakijionesha kwa wadau wao katika utendaji wao ndio hatua mojawapo ya kutangaza ubunifu na huduma wanayotoa.

“Hapa tunawapa cheti na zawadi za kuwatambua lakini haimaanishi kuwa katika Maisha ndio mnatambulika kuwa bora, jambola msingi ni kwamba huduma mnayotoa ndiyo itakayowatangaza,” amesema  Profesa Ndomba.

Habari Picha 10495

Amewataka wanafunzi wanaosoma DIT kuzingatia maelekezo kutoka kwa walimu na zaidi kuwa na nidhamu, uchapakazi na ustahimilivu ili kuwa na mchango  kwa Taifa.

 

 

 

Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.