Na Lucy Ngowi
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi, akiwemo Tido Mhando kuwa Mshauri wa Rais wa Masuala ya Habari na Mawasiliano.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, amesema hayo leo, Novemba 19, 2025, kupitia taarifa kwa umma.
Taarifa hiyo pia imethibitisha kuwa Bakari Machumu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, kuchukua nafasi ya Sharifa Nyanga aliyepewa majukumu mengine.
Aidha, Rais Samia amemteua Lazaro Nyalandu kuwa Balozi.

