MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kutofuata sheria chanzo kikuu cha migogoro ya kazi – CMA
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kutofuata sheria chanzo kikuu cha migogoro ya kazi – CMA
Habari

Kutofuata sheria chanzo kikuu cha migogoro ya kazi – CMA

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: OFISA Mfawidhi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mkoa wa Dar es Salaam, Yohana Massawe, amewataka waajiri kote nchini kufuata taratibu za kisheria wakati wa upunguzaji wa wafanyakazi ili kuepuka migogoro ya kikazi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Massawe amesema CMA imekuwa ikipokea malalamiko mengi yanayohusiana na upunguzwaji wa wafanyakazi, ambapo changamoto kubwa inajitokeza katika kutokufuata utaratibu unaoelekezwa na sheria.
“Mwajiri anaweza kuwa na sababu halali za kupunguza wafanyakazi, lakini akishindwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria, hatua hiyo huonekana ni batili,” amesema..
Amebainisha kuwa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2023, kifungu cha 39, kinamtaka mwajiri anayetaka kupunguza wafanyakazi kutoa taarifa rasmi na muhimu kwa wafanyakazi wake, kisha kuandaa vikao vya majadiliano ili kujadili namna bora ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Kwa mujibu wa Massawe, majadiliano hayo yanaweza kusababisha  makubaliano mbadala kama vile kupunguza mishahara (bila kushuka chini ya kima cha chini cha serikali), kubadilisha vitengo vya kazi, au kupanga upya muundo wa taasisi, badala ya kuachisha wafanyakazi moja kwa moja.
“Lengo la majadiliano ni kufikia mwafaka unaotekelezeka kwa pande zote. Makubaliano hayo lazima yawe kwa maandishi na yahusishe chama cha wafanyakazi au wafanyakazi wenyewe endapo hakuna chama,” amesema.
Massawe ameeleza sababu kuu za upunguzaji ni changamoto za kiuchumi, kiteknolojia au mabadiliko ya kimuundo ndani ya taasisi, amesema mabadiliko hayo yanaweza kusababisha kupungua kwa mahitaji ya nguvu kazi, kwa mfano pale teknolojia mpya inapochukua nafasi ya kazi za watu.
Hata hivyo, alionya kuwa waajiri wengi hushindwa kuzingatia vigezo vya msingi vya upunguzaji na hivyo kujikuta wakikabiliwa na mashauri mbele ya tume.
“Mara nyingi ushahidi unaonyesha sababu ya msingi ipo, lakini kosa linakuwa ni kwenye utaratibu. Ni muhimu waajiri wakajielimisha kuhusu sheria hizi na kuzisoma mara kwa mara,” amesema.
Kwa mujibu wa CMA, mashauri ya upunguzaji kazi yanapaswa kushughulikiwa ndani ya siku 30 katika hatua ya usuluhishi, kabla ya kuhamia hatua ya uamuzi wa upatanishi endapo hakutakuwa na mwafaka.
Massawe amehitimisha kwa kuwataka waajiri kutumia nafasi yao kuhakikisha migogoro ya kikazi inapungua, kwa kuwa kufuata sheria na majadiliano ya wazi ni njia bora ya kulinda haki za pande zote.

You Might Also Like

Ushirikiano Wa Nchi Za Kiafrika Uthibitike Kwa Vitendo -Dkt. Biteko

Samia Kukagua Barabara Ya Mzunguko, Uwanja Wa Ndege Msalato Kesho

Homa ya nyani mjadala wa dharura kwa mawaziri wa afya Afrika

Tafiti Katika Afya Nyenzo Muhimu

July 10, 2025

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Twendeni Tukapige Kura Ya Ukombozi, CHAUMMA Yahitimisha Kampeni
Next Article Idadi Ya Wagonjwa Wa Magonjwa Yasiyoambukiza Kuongezeka
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?