Na Lucy Ngowi
DODOMA: “HADI sasa tunasimamia hifadhi tatu na maeneo Tengefu 15. Tufanye jumla ya hifadhi kufika 18, ambazo zimegawanyika katika mikoa minne, Tanzania Bara,”.
Ofisa Masoko wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania, Halima Tosiri amesema hayo katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yaliyomalizika jana katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Halima ametaja mikoa ambayo hifadhi hizo zinapatikana kuwa ni Hifadhi ya Kisiwa cha Mafia, Hifadhi za Bahari Dar es Salaam, Hifadhi za Bahari Nazbay Mtwara na Hifadhi za Bahari Tanga.
Amesema mwaka huu 2024, wameweza kuhudhuria maonesho hayo yajulikanayo kama nane nane kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii, kuhusiana na masuala ya uhifadhi wa rasilimali za bahari.
Kuwajulisha wananchi, ” Ni kwa nini tunahifadhi, na ni nini tunahifadhi, na umuhimu wa kuhifadhi lakini pia kuwaambia jamii kwa kuwa ni moja kati ya sehemu ya wahifadhi.