Na Danson Kaijage.
WAKALA wa Vipimo (WMA) imesema kuwa kati ya mafanikio makubwa na ya kihistoria kwa miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan tangu kuwepo kwake, ni kupata ajira za wafanyakazi wapatao 186.
Hayo yameelezwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo, Alban Kihulla alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali iliyopo Madarakani katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.

Kihulla amesema kuwa katika historia ya kuwepo Wakala wa Vipimo haijawahi kuwa na watumishi wa kutosha kama ilivyo idadi ya sasa jambo ambalo litasaidia walaka hiyo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Amesena kati ya watumishi hao walioajiriwa, 150 wameisha kuwa na ajira kamili na 36 wapo katika hatua za usahili.

“Tangu kuanzishwa wakala hiyo ilikuwa na changamoto ya kukosa watumishi jambo ambalo lilikuwa likifanya utendaji kazi kuwa mgumu kidogo tofauti na utendaji wa sasa ambapo watumishi wameongezeka ” amesema
Ili kuthibitisha hilo amesema historia ya Idara ya Vipimo nchini Tanzania inaanza mwaka 1884 hadi 1918 wakati wa utawala wa Kijerumani.
Amesema kuwa wakati huo, Idara ya Vipimo ilikuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani na iliendeshwa na Kamishna wa
“Utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Wakala wa Vipimo unahitaji nguvu kazi ya rasilimali watu ambao watafanya ukaguzi na uhakiki wa vipimo.
Wakala inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuiwezesha kupata ajira za watumishi 186 wa kada ya ukaguzi wa vipimo ambao wataongeza nguvu kwenye jukumu la uhakiki na ukaguzi wa vipimo hapa nchini.
Amesema kwa mwaka 2021/2022 watumishi walikuwa 2 mwaka 2022/23 watumishi walikuwa 7,mwaka 2023/2024,watumishi walikuwa
17 na mwaka 2024/2025 watumishi ni
186.