Na Lucy Ngowi
ENDAPO wafanyazi hawatajituma na kuhujumu nchi, uchumi hautakuwa.
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema hayo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), jijini Dodoma.
Amewataka viongozi wa wafanyakazi kuendelea kupambana na viashiria vinavyorudisha nyuma taifa vya rushwa na ubadhirifu.
“Tujitume kwa maendeleo ya taifa letu. Ni jukumu la viongozi wa TUCTA na vyama shiriki kulisemea hili na kulikemea,tuendelee kupambana na viashiria vinavyorudisha nyuma taifa vya rushwa na ubadhirifu,” amesema Ridhiwani.