MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Pinda ashiriki mazishi ya Jaji Kipenka
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Waziri Pinda ashiriki mazishi ya Jaji Kipenka
Uncategorized

Waziri Pinda ashiriki mazishi ya Jaji Kipenka

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
2 Min Read

Na Penny Yohana

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Geophrey Mizengo Pinda ameshiriki mazishi ya kuuanga Mwili wa  marehemu Jaji Kipenka Msemembo Mussa ambaye alikuwa Jaji Msataafu wa Mahakama kuu ya Tanzania na aliyewahi kushika Nyadhifa mbalimbali Serikalini enzi za Uhai wake ikiwemo Katibu Wa Bunge.

Hafla ya Mazishi yamefanyika leo Tarehe 06 November 2024 katika Kijiji cha Kinampanda Kilichopo katika wilaya ya Iramba Mkoani Singida

Pinda ameshiriki Mazishi hayo akimwakilisha Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye ameeleza kwa masikitiko juu ya kuondokewa na Marehemu. Jaji Kipenka Msemembo Mussa.

Mazishi hayo yametanguliwa na Ibada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Wilayani Kinampanda na kuongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati, Dk. Cyprian Hilinti

Akitoa salamu za rambirambi, Naibu Waziri Pinda amesema kuwa Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Serikali nzima wanaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Pinda amesema marehemu Jaji Kipenka  alikuwa kiungo muhimu cha Maendeleo kwa Wananchi wa Kinampanda enzi za uhai wake alikuwa akishirikiana vema na Dkt Mwigulu katika Shughuli mbalimbali za Maendeleo.

“Nimesimama hapa kwa niaba ya mhe. Mwigulu ambaye anatoa pole nyingi sana kwa familia na ameindokewa kwa maelezo yake na mtu muhimu ambaye kilikuwa Kiungo cha Maendeleo cha Kinampanda”. Amesema  Pinda

Aidha Pinda ametoa wito kwa familia ya Jaji Kipenka hasa watoto wa marehemu kuacha kugombania mali zilizokuwa zinamilikiwa na Marehemu Jaji Kipenka kwani Kifanya hivyo kutawaingiza matatizoni zaidi.

“Kikubwa kwenye familia mtulie wakati wa pito hilo katika kukusanya mali za marehemu”, Amesema  Pinda

“Nimeona baba ana watoto wanne lakini watoto kokote waliko wasisahau Mwenza wa Marehemu Jaji Kipenka yupo hai”. Amesema  Pinda

Marehemu Jaji Kipenka Msemembo Mussa alizaliwa tarehe 28, Desemba 1954 ambapo aliugua kwa muda kabla ya kufariki tarehe 2 November 2024.

You Might Also Like

Hakuna Vituo Bandia vya Kuandikisha Wapigakura:Mchengerwa

Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam

Waziri Jenista akabidhiwa ofisi rasmi na Ummy Mwalimu

Mbunge Wa Kibamba Mtemvu. Ajitokeza Kujiandikisha, Kuboresha Taarifa Zake

Kapinga : Bei ya umeme Tanzania ni nafuu kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rafiki Mkubwa wa Trump, Elon Musk atanufaika vipi baada ya kumuunga mkono?  
Next Article Rais Mwinyi Kuzindua Maabara Nguvu Za Atomi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?