Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa usiku wa leo Aprili 5, 2025 ataongoza harambee ya kuwezesha maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa 2025 kwenye ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yatafanyika mkoani Singida na Mgeni Rasmi anarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Ridhiwani Kikwete, Rais wa Shirikisho la Vyama vyacWafanyakazi (TUCTA), Tumaini Nyamuhokya, Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria harambee hiyo.

