MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Mkuu Asisitiza Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote Vijijini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waziri Mkuu Asisitiza Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote Vijijini
Habari

Waziri Mkuu Asisitiza Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote Vijijini

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewaagiza viongozi wa kisiasa na wa serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wote ili waweze kujiunga na kupata uhakika wa huduma za matibabu.
Dkt. Nchemba ametoa agizo hilo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilolo, Dkt. Rita Kabati, wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.
Katika swali lake, Dkt. Kabati alitaka kujua namna Serikali ilivyojipanga kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa Wote hadi ngazi ya vijiji ili kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na huduma za afya.
Amehoji kuwa, licha ya Serikali kufanya kazi kubwa ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi, bado uelewa wa matumizi ya Bima ya Afya ni mdogo kwa wananchi wa vijijini, hivyo kuhoji mikakati ya Serikali katika kutoa elimu hiyo.
Akijibu swali hilo, Dkt. Nchemba amesema Bima ya Afya kwa Wote ni hitaji la muda mrefu kwa wananchi, ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliamua kupanua wigo wake tangu mwanzo wa uongozi wake kwa kuagiza taratibu zote za kisheria zikamilishwe.
“Ni kweli hatua iliyobaki kwa kiasi kikubwa ni kutoa elimu kwa wananchi. Bima ya Afya ni msingi wa kuwezesha Watanzania wote kumudu gharama za matibabu, hususan kwa wale wenye uhitaji mkubwa wa huduma za afya na wasioweza kumudu gharama hizo,” amesema Dkt. Nchemba.
Ameongeza kuwa jambo muhimu kwa wananchi ni kujiunga na mifumo ya bima itakayoelekezwa na Wizara, huku Serikali ikiendelea kufanya jitihada kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa urahisi, kwa uhakika na kwa kuokoa maisha.
Aidha, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliahidi kuajiri wataalamu wa afya 5,000 ndani ya siku 100, ahadi ambayo tayari imetekelezwa, ambapo wataalamu hao wamepelekwa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali kote nchini.
Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha majengo ya huduma za afya yaliyojengwa yanakuwa na wataalamu wa kutosha ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Vilevile, Dkt. Nchemba amesema jitihada hizo zinaenda sambamba na upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa katika hospitali mbalimbali nchini.
“Zamani vifaa kama CT Scan na MRI vilipatikana Dar es Salaam pekee, lakini kwa sasa vinapatikana katika hospitali za mikoa, hospitali za rufaa na hospitali za kanda,” amesema.

You Might Also Like

MSD, SALAMA Zaunganisha Nguvu Kuboresha Sekta ya Afya SADC

MOI Yaokoa Bilioni 150 Matibabu Ya Kibingwa

DKT. Biteko Ashiriki Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia Zanzibar

Spika Mussa Zungu Atoa Hotuba Baada Ya Kuchaguliwa

TEA, UNICEF na Canada waendeleza mageuzi ya elimu Sikonge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article MBUNGE wa Kasulu Mjini Ahoji Serikali Kuhusu Mradi wa Maji Mwanga B
Next Article Bunge Bonanza 2026 Kuikutanisha Simba Na Yanga Dodoma
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?