Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Ndomba Doran.
Dorani alioongozana na Meneja wa Kanda ya Kati wa ATE, Leonard Mapha alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, leo mchana, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika Wizara hiyo