Lucy Lyatuu
CHAMA Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimesema mtumishi wa Umma anatakiwa kufahamu haki ya rufaa Kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma ya mwaka 2019.
Kimesema mtumishi wa Umma anayo nafasi ya kutafuta haki yake Kwa njia ya rufaa au nafuu nyingine iwapo hajaridhishwa na uamuzi wa Mamlaka ya nidhamu.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Sheria Usalama Mahala pa Kazi wa TALGWU, Twaha Mtengera amesema Hali hiyo inaweza kutafuta huko isipokuwa kutokana naabadiliko ya Sheria husika watumishi wa Umma hawaruhusiwi Kwa mujibu wa kifungu Cha 32A cha Sheria ya utumishi wa Umma kutumia sheria za kazi au nyinginezo mpaka wakamiliashe kwanza utaratibu ulioainishwa chini ya Sheria ya utumishi wa Umma.
Kwa mujibu wa Mtengera kifungu Cha 25 Cha Sheria ya utumishi wa Umma pamoja na sehemu ya sita ya kanuni za utumishi wa Umma za mwaka 2022 zimefafanua utaratibu wa kuzingatia katika suala zima la kukata rufaa.