MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watanzania Watakiwa Kuachana Na Dhana Potofu Kuwa Nishati Safi Ya Kupikia Ni Gharama
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watanzania Watakiwa Kuachana Na Dhana Potofu Kuwa Nishati Safi Ya Kupikia Ni Gharama
Habari

Watanzania Watakiwa Kuachana Na Dhana Potofu Kuwa Nishati Safi Ya Kupikia Ni Gharama

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewataka Watanzania kubadili mtazamo hasi kuhusu gharama ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, ukisisitiza kuwa kwa maendeleo ya sasa ya kiteknolojia, matumizi ya nishati hizo si tu yanapunguza gharama za muda mrefu, bali pia yanaboresha afya na kulinda mazingira.
Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba),  katika Banda la REA, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Jones Olotu amesema dhana kuwa nishati safi ni ghali ni potofu na haina msingi wa kitaalamu.
“Kumekuwepo na dhana kwamba kutumia nishati safi ya kupikia, ikiwemo umeme, ni gharama kubwa ukilinganisha na kuni au mkaa.
“Ukweli ni kuwa sasa teknolojia imeboreshwa sana. Majiko haya ni rafiki kwa mtumiaji, yanapunguza muda wa kupika na gharama za muda mrefu za manunuzi ya kuni na mkaa,” amesema.
Katika kutekeleza agizo la Rais wa Samia Suluhu Hassan, REA imeanza kuhamasisha taasisi zinazolisha zaidi ya watu 100 kutumia nishati safi ya kupikia.
Hadi sasa, maeneo 211 ya Jeshi la Magereza, yakiwemo magereza, kambi, shule, vyuo na hospitali yameanza kutumia nishati safi kwa mfumo wa bayogesi, LPG, gesi asilia na mkaa mbadala.
Aidha, maofisa zaidi ya 280 wa Jeshi la Magereza wamejengewa uwezo kuhusu matumizi sahihi na endelevu ya nishati safi ya kupikia ili kuhakikisha mabadiliko haya yanafanikiwa kwa uendelevu.
REA inasisitiza kuwa mapinduzi ya matumizi ya nishati safi si suala la kifahari bali ni hitaji la msingi kwa maendeleo ya taifa, afya ya wananchi, na uhifadhi wa mazingira. Watanzania wote wanahimizwa kutembelea Banda la REA katika Maonesho ya Sabasaba kujionea teknolojia hizi na kujifunza kwa vitendo njia mbadala, salama na nafuu za kupikia.
–

You Might Also Like

Kamati Ya Bunge Yahimiza Maslahi Ya Watumishi Wapya Yazingatiwe

CHAUMMA kuanzisha mjadala wa elimu ndani ya siku 100

TOSCI: Mbegu Bora Ni Ajira, Biashara

Waendelezaji Majengo 103 Kesi Ziko Mahakamani, -AQRB

Serikali Yazindua Mafunzo Ya Mtandao Ya Afya Moja

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wananchi Waelimishwe Kuhusu Utendaji wa Kamati za Maadili za Maofisa wa Mahakama
Next Article FCC Yatoa Elimu Ya Ushindani Wa Kibiashara Katika Maonesho Ya  Biashara
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mita  Janja Zazinduliwa,  Tanesco  Yatakiwa Kuzisambaza Nchi Nzima
Habari December 5, 2025
DIT Andaeni Taarifa  Itakayowezesha Wanafunzi Kupelekwa Nje Kujifunza-Mkenda
Habari December 5, 2025
Msama Aipongeza Hotuba Ya Samia, Atoa Neno Kwa Vijana, Wazee, Wanaharakati
Habari December 4, 2025
Profesa Silayo Aaga, Jawara Kuchukua Uongozi Mpya wa AFWC25
Habari December 3, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?