Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani na umoja ili kujenga jamii yenye ushirikiano na upendo katika Taifa.
Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Septemba 22 , 2024 wakati akizungumza na waumini katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la AICT Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.