MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watafiti Wa Mimea Vamizi Watua Serengeti
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watafiti Wa Mimea Vamizi Watua Serengeti
Habari

Watafiti Wa Mimea Vamizi Watua Serengeti

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu,Serengeti

ZIARA  ya kikazi ya watafiti wa mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba walioungana na wataalam wa ikolojia kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti inatarajiwa kuwa neema kubwa kwa Wanyamapori kwenye hifadhi hiyo.

Ziara hiyo inatarajiwa  kuongeza maeneo ya malisho kwa wanyama hao ambayo kwa sasa yameanza kuathiriwa na mimea vamizi.

Akizungumza na watafiti hao katika Hifadhi hiyo ya kipekee duniani, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Stephano Msumi ameushukuru na  kuupongeza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua hiyo muhimu ya kuwakutanisha watafiti wa Wizara hiyo  kutoka nchini Cuba kutembelea Hifadhi  hiyo na kujionea changamoto hiyo kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wakudumu.

Aidha, amesema  Hifadhi hiyo ni moja ya Hifadhi za Taifa zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kupitia utalii hususani wa Wanyamapori hivyo jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha Wanyamapori wanapata malisho ya kutosha ni za  kuungwa mkono.

Ameongeza kuwa, zipo juhudi zinazofanywa na wataalam kutoka katika Hifadhi hiyo za kupambana na mimea vamizi lakini bado hazijazaa matunda yaliyotarajiwa.

Amesema uwepo wa watafiti hao kutoka Cuba na kuungana na watafiti wa Wizara hiyo ni hatua muhimu katika kufikia malengo ya kuhakikisha malisho na usalama wa ikolojia ya Hifadhi hiyo ni endelevu.

Naye mtaalam mtambuzi wa mimea asili kutoka nchini Cuba, Dkt. Ramona Oviedo Prieto ametoa ushauri kwa wataalam wa ikolojia  wa Hifadhi ya Taifa Serengeti kuchukua hatua za haraka za kulinda kingo za Mto Mara uliopo ndani ya Hifadhi hiyo kwa kurejeresha mimea ya asili iliyokuwepo pembezoni mwa Mto huo.

Wakiwa kwenye Hifadhi ya Taifa Serengeti, timu hiyo ya watafiti walitembelea maeneo ya Seronera, Ikoma, Mto Mara na Machochwe na kushuhudia  mimea vamizi aina ya gugu karoti ( Parthenium hysterophorus) Chromolaena odorata na Opuntia ambayo ndio imeanza kusambaa kwenye maeneo hayo.

 

You Might Also Like

Timu Ya Watanzania Ikiongozwa Na Profesa Ndunguru, Yakutana Na Balozi Zambia

Elimu Ya Dawa Za Kulevya Kutolewa Kwa Wanafunzi

Kanisa La GCC Kufanya Maombi Kuelekea Uchaguzi Mkuu

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda Atoa Neno Kwa Vijana, Maadhimisho Miaka 30 VETA

Bashungwa Asema Wafungwa Kupewa Mafunzo Ya Ufundi Stadi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Sekta Binafsi Kuimarisha Huduma Za Fedha Nchini
Next Article Mpulla: Serikali Imetekeleza Hoja Za TUCTA Kuiboresha CMA
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tume ya Kurekebisha Sheria Yaelimisha Umma Kuhusu Haki za Wanyama
Habari August 6, 2025
Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari August 6, 2025
Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
Mbinu Mpya za Kilimo kwa Vijana Zapata Umaarufu Nanenane Banda La VETA
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?