Na Lucy Lyatuu
SERIKALI inawataka wanawake nchini kutumia mianya inayotengenezwa ya kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara Ili waweze kusambaa kwa kuwafikia masoko m alimbali ndani na nje ya nchi.
Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum ,Felister Mdemu (anayeshughulikia dawati la wanawake na jinisa)amesema hayo Dar es Salaam katika ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake 40 kutoka nchi za Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu huduma na sheria mbalimbali za manunuzi kijinsia.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Kituo Cha Kimataifa Cha Biashara (ITC) chini ya Mwavuli wa kuwaangalia wanawake wajasiriamali duniani (SHE TRADE)na kuratibiwa na Baraza La Biashara la Afrika Mashariki (EABC).
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira mazuri Kwa wanawake kuingia kwenye biashara kwamba ipo mikopo ya asilimia 10 ambayo wanaweza kuvitumia kibiashara na kukuza uchumi pamoja na kuleta familia.
Amesema mafunzo hayo yamewakutanisha wanawake wafanyabiashara wanEAC kubadilishana uzoefu,Kwa kuwa wanawake wa Tanzania wanataka kufunguliwa zaidi kuoneahwa njia za kufanya biashara Kwa sababu mianya Iko wazi
.
” Tumekutana ili kufundisha sheria za manunuzi nchini Kenya zikoje,Uganda,Burundi ili walitaka kuingia humo wawe tayari,” amesema.
Amesema kupitia mafunzo hayo yatawezesha Watanzania kufunguliwa njia, kuoneahwa mianya na kujifunza zaidi bila kuvunja taratibu na kanuni.
Kwa upande wake Meneja wa Biashara EABC, Frank Daffa amesema lengo la mafunzo ni kuwafundisha wanawake kuhusu huduma na sheria mbalimbali zilizoko kwenye mrengo wa manunuzi kijinsia.
“Tunataka kuwawezesga wanawake kupata taarifa lakini pia kujiunga na mitandao mbalimbali ya wanawake iliyo chini ya ITC ili waongeze ufanisi wao wa kufanya biashara kwenye soko la Kimataifa”,amesema.
Amesema wapo wanawake wafanyabiashara 40 pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali za watoa huduma Kwa lengo la kuelimisha wanawake kwamba Kuna fursa Gani ambazo zina mrengo wa kijinsia haswa Kwa wanawake.
Aidha pia wapo wadau wa Mamlaka za ununuzi ambao wataeleza sheria mbalimbali zilizopo kwenye nchi zao ambapo wametoka nchi za EAC ili kuwafundisha wanawake sheria zilizopo na zinavyoweza kuwasaidia wanawake kupata huduma na kufanya manunuzi kama wanawake.
Naye Filis Wanjiru kutoka ITC hususan chini ya Mwavuli wa SHE TRADE, amesema wanatarajia kutengeneza chombo (hb) katika maeneo mbalimbali Ili kusaidia biashara Kwa nchi zinazokuwa Ili kwenda Kimataifa zaidi.
Amesema mafunzo yanavyotolewa Kwa wanawake yanahusu manunuzi ambayo niuhimu kwani Kimataifa wanawake huweza kufanya zabuni Kwa asilimia Moja TU hivyo kupitia mafunzo hayo yatawezesha wanawake kuongeza wigo zaidi wa biashara.
Rais wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Mercy Silla amesema kupitia mafunzo hayo wanawake wake sheria za manunuzi zinavyofanyika pale wanapotaka kufanya biashara.